Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Abel Makubi,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Upimaji na Metrolojia kutoka TBS Mhandisi Johanes Maganga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Dodoma sekta ya uchumi Bi Aziza Mumba,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Mkuu wa Huduma za Ufundi wa Vifaa Tiba-MOHCDGEC Mhandisi Valentino Mvaga mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali,akielezea umuhimu wa wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma Dkt.Kembo Bwana,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Meneja Kanda ya Kati kutoka TBS Bw. Nickonia Mwabuka,akizungumzia umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Abel Makub,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imelitaka Shirika la Viwango nchini (TBS) kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na wapi wapate hivyo vipimo sahihi.

Hayo yameelezwa leo Mei 20 2021 jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Abel Makubi wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vipimo duniani.

Dkt.Kihologwe amesema TBS ina wajibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na wapi wapate hivyo vipimo sahihi kwani wengi wamekuwa wakikutana na wakati mgumu kujua vinapatikana wapi.

“Nitoe wito kwa TBS kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na wapi wapate hivyo vipimo sahihi.Tunafurahi kwamba taasisi zimezungumza ninyi ni walinzi wa Taifa mnaweka viwango vya ubora lakini pia mnasimamia hivi viwango na si viwango tu hata wazalishaji nao pia mnawasimamia,”amesema.

Amesema Wizara ina wajibu wa kuonesha kwamba sera, sheria ,kanuni na taratibu zinafuatwa katika masuala ya vipimo kwa kuhakikisha mtoa huduma na elimu na ujuzi pamoja na maarifa ya kutosha kuhusina na kupima.

“Swali lingine ambalo tunapaswa kujiuliza ni hivi vifaa tunavyovitumia ni sahihi ni wajibu wa sisi wenye mamalaka kusimamia pamoja na kuhakikisha wanaotoa huduma na vifaa vyao vinaruhusu kufanya vipimo.Ni muhimu kujua nani anafanya hiyo huduma nimefurahishwa sana na taarifa ya Mkuu a chuo kwamba wanataka kujenga maabara ya kisasa nami nawapongeza sana.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Upimaji na Metrolojia kutoka TBS,Mhandisi Johanes Maganga ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt.Athuman Ngenya amesema Shirika la Viwango Tanzania ,licha ya kuwa dhamana kubwa ya kuthibiti ubora wa bidhaa nchini na kutoka nje ya nchi pamoja na kumlinda mlaji pia ndio mlezi wa viwango vya Taifa vinavyotumika katika vipimo.

“Vipimo vinaathiri afya zetu mfano unapoenda dukani kununua panadol mbili kwa ajili ya maumivu ya kichwa dawa hizi zinapaswa kuwa katika uzito wa miligramu 500 kwa kila kidoge.

“Viwanda vinavyozalisha vinapaswa kuhakikisha kidonge kimoja hakizidi wala kupungua uzito ili kulinda afya ya watumiaji na ukienda kununua na ukikuta mtengenezaji ametengeneza chini ya hapo akakupa chini ya Milgramu 450 inamana ukikinunua inawezekana kisiende kutibu ule ugonjwa,”amesema.

Vilevile,Mhandisi Maganga amesema huduma bora za afya zinawezekana kwa ubora wa vipimo ambao unatolewa hivyo kwa sasa TBS ina uwezo wa kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za upimaji,uzito,urefu,hali joto ujazo mdogo na mkubwa,muda na masafa mgandamizo

Naye,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Aziza Mumba amesema Vipimo ni muhimu na mtambuka hivyo siku hiyo inatakiwa kutumiwa vizuri kwa wananchi kuelimishwa baadhi ya mambo ambayo hawajui kuhusu vipimo.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: