MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema pamoja na serikali kuja na sera ya elimu bure kwa kuweka uwekezaji mkubwa kwenye miuondombinu lakini iwapo hawatatilia mkazo suala la lishe shuleni jitihada zote hizo zitakuwa hatarini.

Aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni kwa sababu kati ya watoto 45 kati yao 15 hawafundishiki kutokana na tatizo la lishe duni.

Alisema kwa sababu watoto wanapokuwa darasani lazima aweze kufikiri,kuchakata ,kuelewa ,kukariri anachofundishwa na mwalimu lakini kama ubongo wake haufanyi kazi vizuri na hautajapata virutubisho sahihi mtoto huyo hawezi kujifunza ipasavyo na hivyo ni sawa na kutegemea gari ambalo halina mafuta liweze kutembea.

“Mh Spika wanafunzi wengi wanatoka nyumbani alfajiri wanakuwa hawajala wanakwenda shule wanashinda njaa akiwa darasani tumbo linanguruma kwa sababu linakosa kitu cha kusaga na kupeleka kwenye ubongo kwa hiyo mwanafunzi anakosa umakini kiasi kwamba mwalimu anatoka kufundisha ukimwambie mwalimu kasema nini akasema sijui mtoto unaangaika kumpiga kwa kusema ni mtoto mtukutu hana adabu hasikilizi darasani lakini ubongo wake umesizi kufanya kazi kwa sababu ya njaa”Alisema Mbunge  Neema Lugangira

“Lakini Mh Spika ningependa kuikumbusha serikali kwamba  pia hali udumavu nchini inachangia kwa kiasi kikubwa kwa watoto kutokuweza kufaulu na kutokufundishika shuleni…wenzetu wataalumu wa lishe Tamisemi wanasema kwamba  kila darasa la watoto 45 kati yao 15 hawafundishiki inaamaana pamoja na jitihada zote hizo tunaendelea kufifisha jitihada kutokana na uelewa ndio maana ufaulu unakuwa chini.”Alisisitiza Mbunge Neema Lugangira

Mbunge Neema Lugangira alisema kutokana na hali hiyo aliiomba serikali iweke mikakati madhubuti kuhakikisha ya kila shule hususani za kutwa wanazalisha mazao ya lishe ili kuhakikisha watoto hawashindi shuleni wakiwa na njaa.

 “Pia niseme kwamba pamoja na jitihada zote za elimu bure,miuondinu bora ikiwa bado tutaliweka pembeni suala la lishe shuleni jitihaza zote zitafifisha malengo ya serikali ya kuhakikisha elimu yetu inanufaisha watoto wa kitanzania kwa hiyo naiomba wizara ya elimu sayansi na tenkologia ije na mkakati madhubuti tunakwenda kufanya nini kuhakikisha watoto wanapata lishe shuleni”Alisema

Akizungumzia suala la Hedhi Salama  Mhe Neema Lugangira alianza kwa kuipongeza Serikali kwa mikakati waliyoweka kuhakikisha mtoto wa kike analindwa ili apate elimu lakini mtoto huyo huyo kila mwezi anapofika wakati wa hedhi anakosa siku tano mpaka saba.

Alisema kutokana na  hali hiyo  anaiomba serikali itilie mkazo nafahamu kuna bajeti ndogo ya elimu bure kupata msaada wa taulo za kike kwa dharura lakini serikali iweke wazi lakini waje na mikakati madhubuti kwenye eneo  hili.

“Kwa mfano kwenye shule za msingi kuna wanafunzi wa kike 5,481,982 na sekondari wa kike 1,284,410 kati ya hao wote tukichukulia asilimia 20 wapo kwenye umri wa kubalee inamaana tuna jumla ya watoto 2,380,806 ambao kila mwezi wapo hatarini kukosa shule siku tano mpaka saba hilo ni jambo nzito inabidi wizara ilichukulie kwa uzito wa kipekee kuona namna ya kukabiliana nalo”Alisema

Hata hivyo Mbunge Neema Lugangira alisema lakini kwa wale wanaoenda shule wanatumia vitu ambavyo ni hatari kwa afya zao kwa hiyo anaiomba serikali ione namna gani inaweza kusaidia mtoto wa kike kwa kuhakikisha akosi shule kwa sababu ya kuwa kwenye hedhi .

“Lakini kwa kumalizia naamini kwa sababu Waziri ni Mama yetu na hayo masuala yote mawili yanamgusa kama mama naamini atakuja na mpango mazubuti wa kuhakikisha watoto wanapata lishe shuleni pia mtoto wa kike hakosi shule kwa sababu anakuwa kwenye hedhi”Alisema

Kufuatia suala hilo Spika wa Bunge Job Ndugai ameweza kulizungumzia ambapo alisema kwenye suala la lishe kwa mfano maeneo mengi ikiwemo Jijini Dodoma na maeneo mengine shule zina eneo kubwa  la kulima ya ardhi lakini unakuta haina magunia mawili ya mahindi au mtama  kwa sababu ya sera ya sasa watoto wasichangamke na kidogo na vijembe.

Spika Ndugai alisema lakini katika maeneo yao ya shule wangeweza kila shule kujipanga na kulima kwa kupata wastani wa magunia 50 hadi 70 kwa kuanzia kabla ya hata wazazi wao hawajachangia chakula shuleni.

“Lakini mtoto umechukua na umempeleka shuleni na mzazi umempungiza nguvu kazi ya kufanya kazi nayo nyumbani amehaingaika peke yake na kiangazi kikifika unamwambie mzazi achukule chakula apelekea shuleni hivyo ni vitu vya kutazama kwani baadhi ya vitu ni kujipanga tu kwa sababu ardhi ipo”Alisema Spika Ndugai

Mwisho
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: