Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi nne za Dodoma Jiji ambazo ni Shule ya Msingi Kisasa,Medeli,Kizota na Mlimwa C.
Mradi huu ambao unagharimu kiasi cha Tsh 1,902,000,000 (Shilingi Bilioni Moja Milioni Mia Tisa na Mbili) umelenga katika kutatua changamoto ya madarasa ya kusomea na matundu ya Vyoo katika Shule hizo.
“Ninaishukuru Serikali chini ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ukarabati na ujenzi wa matundu ya vyoo ambazo kwa kiasi kikubwa zitapunguza adha kwa wanafunzi wetu wa Shule za Msingi.
Mradi huu umekuja wakati wa muafaka hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa mahitaji ya vyumba vya kusomea kwa wanafunzi ni makubwa sana hali inayosababishwa na muitikio wa sera ya Elimu bure na kuhamia kwa serikali Jijini Dodoma.
Natoa rai kwa kamati za shule kuhakikisha wanasimamia ipasavyo fedha za mradi huu kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili matokeo ya mwisho ya lengo lililokusudiwa yaonekane”Alisema Mavunde
Akishukukuru kwa niaba ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma toProf. Davis Mwamfupe ameishukuru serikali kupitia TEA kwa mradi huu mkubwa na kuahidi kuendelea kutenga bajeti kubwa ya Elimu kwenye miradi ya maendeleo ili kupunguza changamoto za kwenye sekta ya Elimu.
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye amewata wadau wote wahusika wa usimamizi wa mradi huo kuhakikisha kazi yote inakmilika ndani ya miezi minne(4) ili kuwapa fursa wanafunzi kuanza kutumia miundo mbinu hiyo kwa wakati.
Post A Comment: