Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akizungumza na wafanyabiashara wa  Nyama katika machinjio ya Vingunguti mara baada ya kukagua machinjio mapya na yale ya zamani leo Mei 17, 2021 Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa jijini la Ilala juu ya ujenzi wa vizimba vya wafanyabishara katika machinjio ya Vingunguti Mkoa wa Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa machinjio mapya ya kisasa yaliyopo Vingunguti mkoa wa Dar es Salaam wakichuna Mbuzi, ambao wamechinjwa kwa mfano katika machinjio hayo ya Kisasa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, Dkt.Angelina  Mabula akizungumza leo katika machinjio ya Vingunguti.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo  amefanya ziara katika Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam yanayojengwa na shirika la nyumba la Taifa(NHC).

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu amejionea namna ya Machinjio  hayo yalivyo na uwezo kuchinja Ng'ombe 1000 na Mbuzi 1500 kwa muda wa saa 24.

Akizungumza Mara Baada ya kutembelea Machinjio hayo Waziri Mkuu ameagiza pande zote mbili za  soko hilo kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija kwa jamii kwa ujumla.

"Nimesikiliza pande zote naagiza kuanzia sasa muendelee kuwa na mazungumzo yapamoja hili kuleta tija katika uendeshaji wa Machinjio haya bila ya mtu kulalama." Amesema Majaliwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, Dkt.Angelina  Mabula amemuhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kuwa ujenzi uliobaki wa Machinjio hayo utakamilishwa mapema Kama NHC walivyohaidi.

Amesema kuwa kazi ya ujenzi wa viyoyozi na vizimba utakamilishwa huku zoezi la uchinjaji likiwa limeanza.

Nae Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonah Kamoli ameomba Waziri Mkuu kuwaagiza viongozi wanaosimamia Machinjio hayo kutoa vipaumbele vya ajira kwa wakazi wa vingunguti na Jimbo la Segerea.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: