a. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye Ofisi yake mpya iliyopo eneo la Mji wa Serikali –Mtumba jijini Dodoma leo, baada ya kuapishwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 01,2021 Ikulu ya Chamwino kushika wadhifa huo.
                                      
Na John Mapepele, Dodoma
Naibu
 Waziri wa Habari Utamaduni na Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Philipo  
Gekul ameomba  ushirikiano  baina Viongozi Wakuu wa Wizara, Watendaji na
 Watumishi wote wa Wizara ili kutekeleza majukumu ya Wizara  hiyo 
kimamilifu kulingana na  Miongozo  ya Serikali, Maelekezo ya Mheshimiwa 
 Rais na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hatimaye matarajio ya 
wananchi yaweze kufikiwa. 
  
Mhe.
 Gekul ameyasema haya  alipowasili rasmi leo kwenye Ofisi yake mpya eneo
 la Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma  mara baada ya kuteuliwa na 
Mheshimiwa Rais  kwenye nafasi hiyo  hivi karibuni akitokea Wizara ya 
Mifugo na Uvuvi ambako alikuwa akihudumu kwa nafasi hiyohiyo. 
  
“Mheshimiwa
 Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara,  madaraka  haya 
tuliyopewa ni sawa na makoti ya kuazima  hivyo  tuna kila sababu ya 
kumtanguliza Mungu na kuimarisha ushirikiano ili kuleta  matokeo 
tarajiwa  kwa wananchi wetu wakati tunatekeleza majukumu yetu ya kila 
siku” amesisitiza Mhe. Gekul 
Amemshukuru Mheshimiwa Mama Samia 
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumwamini  na
 kumrejesha tena  kwenye  nafasi hiyo pamoja na  viongozi wote Wakuu wa 
Wizara hiyo ambapo ameongeza kuwa hali hiyo itarahisisha  utekelezaji wa
 majukumu  ya Wizara kwa ufanisi  kwa kuwa watendaji wote wamerejeshwa 
na wanauzoefu wa kutosha. 
Amemhakikishia Waziri Bashungwa 
kufanya kazi kwa bidii ya kumshauri na kumsaidia kwa kadiri ya uwezo 
wake wote kama msaidizi wake. 
Kwa upande wake, Waziri wa Habari,
 Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Watumishi 
wote kuwa na mshikamano wa  hali  ya juu ambapo amesisitiza watumishi 
wasisubiri  kusukumwa na Katibu Mkuu na badala yake wachape kazi ili 
kukidhi  dhamira  ya Mhe. Rais ya kuwatumikiwa wananchi kikamilifu. 
“Napenda
 kusema tukigundua mahali popote kwenye Wizara yetu  hakuna ushirikiano 
tutachukua hatua mara moja  maana hiyo itakuwa  ni hujuma kwa 
taifa”amefafanua  Mhe. Bashungwa 
Amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa
 kumwamini na kumteua tena kuendelea kusimamia Sekta zilizo chini ya 
Wizara hiyo pia kumteua Mhe. Gekul kuja kuongeza nguvu katika kutekeleza
 na kumuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kutekeleza 
Ilani  ya CCM na hotuba aliyoitoa awali kama  mwongozo kwa Watendaji 
wote wa Serikali. 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi
 amemshukuru Mhe.Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua 
kwa mara  nyingine  kuwa Katibu Mkuu na kumwahidi  kushirikiana na 
Viongozi na Watumishi  wote kutekeleza  majukumu ya Wizara kwa weledi  
na kuzingatia taaluma. 
Akizungumza kwenye Kikao cha Menejimenti 
ya Wizara hiyo mara baada ya kupokea maelekezo ya Waziri Bashungwa, Dkt.
 Abbasi   amesisitiza watendaji wa Wizara kutoka na kuwa jirani na wadau
 wa sekta zilizochini ya Wizara hiyo kwa kuwa wanahitaji kulelewa kwa  
karibu. 
Amesema jukumu la Wizara ni  kuzisimamia sekta zilizo 
chini ya wizara  hiyo kikamilifu kwa weledi ili kupata matokeo chanya 
kwa kuwa nchi yetu imebahatika  kuwa na wasanioi wenye  vipaji na vipawa
 vingi  kinachotakiwa ni usimamizi madhubuti.




Post A Comment: