Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu jana 25/4/2021 ametoa mabati 142 yenye thamani ya Shilingi 4,828,000/= aliyoahidi wakati wa kampeni kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi Mkurumuzi  Kange Kata ya  Maweni.


Mh. Ummy amekabidhi mabati hayo mbele  ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga ndugu Daudi Mayeji na viongozi wengine wa kata na mtaa wa Kange.


Aidha mhe Ummy ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi wa Kange na Maweni kwa ujumla kwa kumchagua yeye kuwa mbunge wa Jimbo la Tanga, na mhe. Colyvas kuwa diwani wa kata ya Kange na Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliekuwa Rais wa awamu wa 5 ambae Mungu amempenda. Mhe Ummy ameeleza kuwa sasa Rais Samia ameshiks usukani wa nchi na hivyo hatuna budi kumuombea na kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake. Mhe Ummy ameeleza kuwa katika mwezi huu April 2021, tayari Rais Samia ameleta shilingi milioni 660 kwa ajili ya kujenga madarasa na vyoo katika Shule za Msingi za Msala, Mapambano, Kasera, Jaje na Bombo na Shule za Sekondari za Kirare,Macechu,Mikanjuni, Mnyanjani na Tongoni pamoja na ujenzi wa bweni la sekondari MACECHU.


Shule ya Mkurumuzi ina jumla ya wanafunzi 1,075  kuanzia darasa la awali hadi darasa la Saba. Kwa mwaka 2021 wanafunzi wa awali walioandikishwa ni 88 na darasa la kwanza ni 162. Baadhi ya wanafunzi wanatembea umbali mrefu zaidi ya km 3 hivyo kusababisha mahudhurio ya wanafunzi kuwa hafifu, Usalama mdogo wa wanafunzi hasa wa awali na darasa la kwanza.


Baadhi ya wananchi walimpongeza mhe mbunge kwa kutekeleza ahadi zake. Pia kwa kuteuliwa kuwa Waziri Wa Tamisemi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: