MBUNGE
 wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) 
Mh Neema Lugangira akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo wakati wa 
kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na 
Kumpongeza Mhe Rais Samia MBUNGE
 wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) 
Mh Neema Lugangira Bungeni Jijini Dodoma wakati wa 
kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na 
Kumpongeza Mhe Rais Samia 
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
 wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) 
Mh Neema Lugangira amesema Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) hapa nchini 
zitampa ushirikiano mkubwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika 
kutekeleza Dira na mipango yake ya maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Mh
 Neema Lugangira ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa 
kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na 
Kumpongeza Mhe Rais Samia ambapo pia alisema kwamba wiki hii Asasi zaidi
 ya 200 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimewasilisha tamko la pole na 
salamu za Pongezi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassani ikiwemo Jukwaa la 
Wanawake Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) nao wametoa tamko
 la pongezi kwa Rais.
Alisema
 kwamba Sekta ya Asasi za Kiraia ina imani kubwa sana naye kwa sababu 
anauzoefu mkubwa sana wa uongozi na mafanikio lukuki ambayo yatawezsha 
kuleta tija kubwa kwa maendeleo ya Taifa letu la Tanzania
“Lakini
 nitumie fursa hii kutaja maeneo machache: Mhe Rais Samia Suluhu Hassan 
alianza ajira yake kwenye mwamvuli mashirika yasiyokwa ya kuserikali 
linaloitwa ANGOZA (Association for Non Governmental Organisations in 
Zanzibar) hivyo ni mwana Azaki mwezetu na ana uzoefu mkubwa ambao 
utakuwa chachu kwetu”Alisema
Mbunge
 Neema alisema Rais Samia anauzoefu mkubwa sana kwenye masuala ya 
uwezeshwaji kiuchumi na kupitia uzoefu huo mwaka 2016 Katibu Mkuu wa 
Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alimteua Rais Samia akiwa Makamu wa Rais 
kuwa Mjumbe wa Jopo la Dunia kama Mwakilishi wa Afrika la kumshauri 
namna bora ya kufanikisha Uwezeshwaji Wanawake Kiuchumi.
Alisema
 la tatu ni kwamba miaka 25 iliyopita Rais Samia akiwa anatokea kwenye 
NGOs alishiriki kwenye Mkutano wa Beijing uliokuwa unalenga kuleta 
ukombozi wa usawa na kijinsia ikiwemo wanawake kwenye nafasi za uongozi 
na maamuzi.
Aidha alisema
 kupitia yeye kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Tanzania ameiwezesha 
Tanzania kuweka historia ya kuwa sehemu ya Utekelezaji wa Maazimio ya 
Beijing 
Mbunge Neema 
aliongezea kuwa akiwa kama mdau wa lishe wao wanatambua kuwa juhudi 
kubwa ambazo Mhe Rais Samia ameweka katika kuhakikisha Serikali 
inaboresha hali ya lishe hapa nchini.
Mbunge
 huyo alisema vivyo hivyo wanatambua jitihadi kubwa za Makamu wa Rais 
Mteule, Mhe Dkt Philip Mpango ameweka kwenye kuboresha hali ya lishe kwa
 kuhakikisha kwamba Halmashauri zinatenga bajeti ya lishe kwa kulingana 
na idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Mh
 Naibu Spika napenda kuwasilisha ombi rasmi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan la kukutana na Sekta ya Asasi za Kiraia  ili nasi pia tuwe sehemu ya mafanikio yake”Alimalizia Mbunge Neema 
Lugangira
MWISHO



Post A Comment: