Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Izack Amani akisaini kitabu cha msombolezo kilichopo katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Meneja msaidizi wa Benki ya Azania Tawi la Arusha,Yusufu Lenga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofika kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Afisa mahusiano wa Benki ya Azania Tawi la Arusha,John Machota akieleza namna ambavyo atamkumbuka hayati Dkt.John Magufuli katika masuala mazima ya kimaendeleo.

 

 

Na Jusline Marco-Arusha

Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Izack Amani amesema kuwa watamkumbuka  na kumuenzi hayati Dkt.John Magufuli kupitia kazi alizozifanya kwa watanzania kwa vile alivyokuwa jasiri na mwenye kuthubutu katika uletaji wa maendeleo na kufungua ukurasa mpya kwa watanzania.

Akisaini kitabu cha Maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Askofu Amani amesema kupitia yale aliyoyafanya hayati Dkt.Magufuli watanzania wanapaswa kujifunza kufanya kazi kwa uaminifu wakati wakiwa na muda huku wakiomba neema ya kutumia muda huo vizuri na kuchangia vipaji vyao kwa ukarimu kwa maendeleo ya nchi.

       "Hayati Dkt.Magufuli alifungua ukurasa mpya kwa Tanzania na kuandika historia mpya,mabadiliko makubwa ya ujasiri na uthubutu na kuona kwamba kila kikundi kinashiriki furaha ya uhuru."Alieleza Askofu Amani

Pamoja na hayo Askofu Amani amewataka watanzania kutambua kuwa Mungu amemuumba mwanadamu kwa malengo na kuweka ndani tamaa ya maendeleo na kuwapatia vipaji na karama mbalimbali hivyo wanapaswa kuendelea kumshuru Mungu kwa yote waliyojaliwa na kuwa na roho ya ushirikiano kuanzia ngazi ya famili,jamii na taifa kwa ujumla.

       "Tujifunze kwa hayati Dkt.Magufuli kuwa alikuwa na nia njema na amejitolea kwa ajili ya kusaidia watu wote kwa tabaka tofauti tofauti,ule ukarimu wa kumrudishia shukurani kupitia kuwatumikia watu kwa upendo na uaminifu huku tukiepuka utoaji na upokeaji wa rushwa."Alisisitiza Askofu Amani

Katika hatua nyingine Uongozi wa Banki ya Azania Tawi la Arusha umeazimia kumuenzi hayati Dkt.Magufuli kwa kile alichokifanya enzi ya uhai wake ikiwemo uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi

Akitoa pole kwa watanzania na familia ya hayati Dkt.John Magufuli,Meneja msaidizi wa Benki ya Azania Tawi la Arusha,Yusufu Lenga amesema kuwa kama taasisi ya fedha watamkumbuka hayati Dkt.Magufuli kwa uanzishwaji wa mahakama za mafisadi na kusaidia watu kuwa na nidhamu ya fedha.

     "Kupitia mahakama ya mafisadi iliyoanzishwa na hayati Dkt.Magufuli kila mtu ameona jukumu lake ni kutafuta fedha halali na kuyafanya maisha ya kibiashara yawe ni maisha ambayo mtu ayafanyi kwa njia za mkato."alisema Lenga

Amesema kutokana na hilo,imesaidia watu wa taasisi ya fedha kutokuwa na fedha nyingi za mashaka lakini pia wanaendelea kukagua kila fedha ambayo huingia kwenye taasisi ambapo asilimia kubwa nidhamu ya wafanyabiashara,wafanyakazi na wengine kwenye sekta ya kifedha imekuwa ya hali ya juu.

Kwa upande wake Afisa mahusiano wa Benki hiyo,John Machota amesema kywa kama taasisi ya fedha ya Azania wataendelea kumkumbuka hayati Dkt.Magufuli kwa kuifanya heshima iwepo serikalini pamoja na utolewaji wa elimu bure ambayo imefanya kila mtoto anapata elimu hiyo pasipo kubugudhiwa.

    "Taarifa za kifo cha Mhe.Rais zilinikosesha usingizi kwasababu niliangalia mambo ambayo ameyafanya na kuyaanzisha katika nchi yetu niliwaza yataendelezwa vipi kweli sikupata usingizi."alieleza Machota

Amebainisha kuwa watamuenzi hayati Dkt.Magufuli kupitia fursa ya kuwapatia elimu bure watanzania ambapo amewataka watanzania kuwa na umoja pamoja na mshikamano katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Mhe.Samia Siluhu na kuamini kuwa ataweza kuwafikisha watanzania kule ambapo hayati Dkt.Magufuli angeweza kuwafikisha.

Share To:

Post A Comment: