Katika  kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kauli mbiu yake ni"Wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa,"Diwani wa kata ya sekei Gerald Sebastiani ametoa mikopo kwa wanawake ili kuwakomboa kiuchumi na kuinua kipato kwa maslahi ya familia na jamii kwa ujumla.


Akitoa mikopo hiyo kwa wanawake 20 ambapo kila mwanamke amepewa sh.50000 ili kujiendeleza kibiashara na kukuza uchumi wa familia zao ikiwa siku ya wanawake imemgusa kutokana na kufahamu umuhimu wa mama katika jamii.


Akizungumza diwani Sebastian alisema fedha hizo zitakaporejeshwa hazitarudi kwenye mikono yake bali zitawafikia wanawake wengine wenne mazingira  magumu ya upatikanaji wa mitaji katika kuendeleza biashara zao ili kujikwamua kiuchumi.


"Mikopo hii haina riba lakini na imani ndani ya miaka mitano naweza kuwashika mikono wanawake 5000 ikiwa kitu hiki kimenisumbua sana kwa muda mrefu kwani ilikuwa ni moja ya ahadi yangu katika kampeni kuwasaidia wanawake,"alisema diwani Sebastian.


Sebastian alisema pamoja na hizo fedha alizowapatia sio msaada bali wakazitumie katika kuendeleza miradi yao midogo midogo ikatumike kuongeza mtaji katika biashara wasivunjike moyo kwani kuna wafanyabiashara wakubwa walioanza na mitaji kama hiyo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuhiya ya umoja wa wanawake wa jiji la Arusha(UWT) Marry Kisaka alisema ni ya diwani huyo ni wanawake kufanya kazi ikiwa asilimia kubwa ya wanawake ni tegemeo kubwa kwa jamii  hivyo mwanamke akijipanga vizuri katika kufanya kazi wataondokana na utegemezi na kuinuka kiuchumi.


"Fedha hizi sio ndogo kwani mimi mwenyewe  nilianza na mtaji wa sh.50000 hadi sasa umekuwa kufikia takribani milioni 30 kwa maana kwamba usidharau kidogo unachopata hivyo wanawake mkasimame imara katika kufanya kazi,"alisema Mwenyekiti huyo UWT.


Afisa maendeleo ya jamii kata ya Sekei,Mecy Urasa alisisitiza kuwa mikopo hiyo iwe chachu ya kuleta maendeleo katika familia na jamii kwa kuendeleza miradi yao midogo midogo ili kuleta tija kwa jamii kwani kwa kuunda vikundi ni njia pekee ya kuwezeshwa kupata mikopo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: