Nteghenjwa Hosseah, Mbeya


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dr. Festo Dugange ameonyesha kutoridhishwa na ukusanyaji wa mapato ya Kituo cha Afya Kiwanjampaka Jijini Mbeya na kuagiza kuimarishaa kwa usimamizi wa kituo hicho ili kudhibiti uvujani wa mapato.


Dr. Festo amesema hayo wakati wa ugawaji wa vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la WRP-T Kwa Mikoa ya Mbeya, Songwe,Rukwa na Katavi mapema tarehe 13.2.2021 kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Kiwanja mpaka.


Akizungumza katika hafla hiyo Dr. Dugange amesema ili Kuboresha huduma vituo vya Afya ni lazima vidhibiti ukusanyajo wa mapato yake ili yaweze kutumika kwenye uendeshaji wa kituo na sio kusubiria fedha kutoka Serikali kuu.


“Nimeanza kwa kikagua kituo hiki cha Kiwanja Mpaka nimeambiwa kuwa makusanyo kwa siku ni shilingi laki tatu ilihali watu wanaotibiwa kwa siku hapa ni mia tatu kwa hesabu za haraka hataka kituo kinatakiwa kukusanya si chini ya shilingi laki sita kwa siku.


Tukadirie kwa siku hiyo moja kuwa wagonjwa mia tatu wanafika kati ya hao mia mbili wanalipia kwa maana ya papo kwa papo, gharama za kumuona Daktari ni shilingi elfu tatu kwa idadi ya wagonjwa hao tu inatakiwa kuwa shilingi laki sita hapo hatujaweka gharama za maabara wala dawa sasa nyie mnaniambia laki tatu hizo Fedha zingine zinakwenda wapi? Alihoji Dr. Dungange.


Bila kutumia akili nyingi utagundua tu kuwa hapa mapato yanavuja na nyie mko tu hamna wasiwasi kabisa hatuwezi kwenda hivyo ni lazima

Mianya hii ya upotevu wa mapato idhibitiwe ipasavyo na mapato yaonekane” alisema.


Aliongeza kuwa “Kituo hiki kiko katikati ya Mji kinatakiwa kiwe na hadhi lakini muonekano wake hauvutii Kituo kimechakaa sana majengo chakavu hata rangi mnashindwa kupiga au kufanya ukarabati mdogo mdogo” alihoji Dr. Dugange.


Aliwataka watalaam wa Afya Jijini Mbeya kujitathmini na kuweka mikakati itakayoleta tija katika utoaji wa huduma bora za Afya Jijini humo.


Katika kutekeleza maagizo hayo alitoa muda wa miezi miwili kwa wataalam hao wa Afya kuhakikisha kuwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vyote Jijini Mbeya unaimarishwa na kuahidi kurudi Mwezi Mei 2021 kukagua utekelezaji wa maagizo hayo.











Share To:

Post A Comment: