Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP Ndugu Mark Tsoxo kutoka Shirika la lisilo la Kiserikali la Heifer International kulia akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki hundi ya Sh.zaidi ya Bilioni 1katika shughuli za maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP Ndugu Mark Tsoxo kutoka Shirika la lisilo la Kiserikali la Heifer International kulia mwenye suti nyeusi na tai nyekundu  akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki hundi ya Sh.zaidi ya Bilioni 1katika shughuli za maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akipokea magari yatakayotumika kwenye mradi wa usambazaji wa maziwa yaliyotolewa na Shirika la lisilo la Kiserikali la Heifer International kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo

ZAIDI ya Bilioni 1 zimetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania (TMPP) ambalo limekuwepo nchini tangu mwaka 1974 likishirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.

Shirika hilo limekuwa likitekeleza shughuli zake za maendeleo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ile ya East Africa Dairy Development Awamuya Pili (EADD II) ambao umekamilika Oktoba 2019 na Mradi wa Usindikaji Maziwa Tanzania unaotekelezwa sasa katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro, Iringa, Pwani, Njombe, Mbeya na Songwe.

Mradi huo unakwenda sambamba na Programu mbalimbali yamaendeleoikiwemoile Tanzania Livestock Master Plan (TLMP), ASDP II na MKUKUTA III ambayo  inatoa dira ya maendeleo katika sekta za Kilimo ikiwemo,Tasniaya Maziwa nchini.

Aidha amesema TMPP inakwenda sambamba na Mkakati Kabambe wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda.

 
Mradi wa TMPP unafadhiliwa na Mfuko wa Wakfu wa Bill & Melinda Gates na Heifer Project International na kutekelezwa na shirika hilo kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa Tasnia ya Maziwa Tanzania.

Lengo kuu la mradi huu ni kuongeza kipato na kuboresha maisha ya wafugaji 50,000 kwa kuwaunganisha na masoko ya maziwa ya uhakika,kuongeza ubora wa maziwa na kusaidia wasindikaji kupata maziwa ya kutosha na yenye ubora unaokidhi viwango.


Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP Ndugu Mark Tsoxo, amesema kuwa kati ya Januari na Disemba 2020, mradi umeweza kuwafikia wafugaji wapatao 47,000 (wanawake asilimia 37%) ambao hupata huduma mbalimbali za ufugaji, elimu na masoko ya maziwa kupitia mradi, wasindikaji maziwa, vikundi na vyama vyao vya Ushirika.

Alisema kati yao wafugaji 45,000 wamepata mafunzo ya ubora wa maziwa na 23,000 wanakusanya maziwa katika vikundi, vituo vya kukusanya maziwa na kwa wasindikaji wa maziwa.

Aliongeza kwamba Mradi huo unavisaidia vyama 82 vya Ushirika katika nyanja za uzalishaji, uongozi bora na uendeshaji biashara ya maziwa.

Vilevile alisema mradi huo umesaidia ongezeko la asilimia 56 ya ukusanyaji maziwa sawa na lita 31,000 kwa siku kiwango ambacho ni zaidi ya lengo la mradi la kufikia asilimia 20 ifikapo Aprili 2021.

Aidha alisema upotevu wa maziwa vituoni umepungua kutoka asilimia 15 hadi chini ya asilimia moja huku akibainisha kwamba viwango vya maziwa yanoyokidhi ubora wa hali ya juu wa bidhaa za UHT umeongezeka kutoka asilimia 30 hadikufikia 90.

Shirika la Heifer International kupitia Mradi wa TMPP limekabidhi msaada wa malori manne maalum ya kubeba maziwa, seti Sita za matenki ya kupoza maziwa na Jenereta Nane zitakazotumika katika vituo vya kukusanya maziwa.

Alibainisha kwamba msaada huo wenye thamani ya takriban shilingi Bilioni 1.088 umetolewa kusaidia kuongeza wigo wa masoko ya maziwa kutoka kwa wafugaji.

Aidha Meneja Fedha wa Mradi huo Ndugu Godlove Mville alifafanua kuwa misaada hiyo imetolewa kwa ASAS, Tanga Fresh, Dar Fresh na Kilimanjaro Fresh ambao wanatengeneza maziwa ya UHT; pamoja na wadau wengine wakiwemo Chama cha Ushirika wa Wanawake Nronga Mkoani Kilimanjaro na kiwanda cha maziwa cha Wahitimu wa SUA cha Shambani Milk kilichopo Morogoro.

Akifanunua ndugu Tsoxo amesema kuwa Heifer International kupitia miradi ya EADD II na TMPP imechangia miundombinu ya ukusanyaji 17 vyenye uwezo wa kupoza lita 60,000 na kuongeza uwezo wa usafirishaji kwa lita 55,000 kwa wakati mmoja.


Awali akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki amelipongeza Shirika la Heifer International kwa kuitikia wito wa Serikali wa kusaidia ujenzi wa nchi yenye Uchumi wa Viwanda na kuinua hali za wafugaji hapa nchini.

Waziri Ndaki ametoa wito kwa mashirika mengine ya maendeleo kuiga mfano wa Heifer International kwa kuwekeza katika mitaji ya maendeleo.

Katika hatua nyingine Waziri Ndaki alisema Serikali kupitia Waziri huyo imeiomba Heifer International kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuleta maendeleo ya Mifugo hapa nchini.Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: