NA HERI SHAABAN
NAIBU MEYA wa halmashauri ya ILALA Saady Kimji aeleza mikakati ya utekeleza wa Ilani 2025.
Naibu Saady Kimji alielezea utekekeza wa Ilani Leo katika chakula cha mchana wakati wa kuwashukuru wajumbe wapiga kura wake wa kata ya Ilala.
Kimji alisema katika utekelezaji wa Ilani mikakati yake kujenga soko la kisasa Ilala na Kituo cha Afya ambapo kata hiyo itakuwa ya kisasa kwa kuboresha huduma za afya.
" Mikakati yangu tunatafuta eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha afya fedha ipo tayari shilingi milioni 200 pia tunajenga soko kubwa la Ilala Boma kutokana na soko lililopo dogo watu wafanyabiashara wengi '"alisema Kimji
Mikakati mingine katika sekta ya elimu kuongeza shule waweze kuwa na kidato cha tano na kidato cha sita awali kata ya Ilala ilikuwa aina Shule ya sekondari Juhudi kubwa amefanikisha Mbunge wa Ilala Mussa Zungu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri katika sekta ya elimu Wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma.
Akielezea ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM aliwapongeza kwa kufanikisha Ushindi kwa asilimia 78 amewataka wajumbe kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo wanapoandaa mikutano Wenyeviti Washirikishe Chama cha Mapinduzi CCM
Aidha pia aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Watendaji kutatua kero ngazi ya mtaa kuisaidia Serikali kwani ni sehemu ya majukumu yao ya kazi wasiyakwepe.
Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Watendaji wawe wadilifu
wafanye kazi kwa bidii waunge mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli katika kujenga TANZANIA ya Uchumi wa viwanda
Kwa upande wake Mratibu wa Polisi Jamii Kariakoo Inspector Mayamba Adam aliwataka wajumbe wa mashina na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa washirikiane kutoa taarifa za waamihaji haramu endapo wataficha kutoa watawashugulikia. Kamanda.
Ispector Adamu aliwata washirikiane katika masuala ya Ulinzi na Usalama katika Kata hiyo
Mwisho
Post A Comment: