Spika wa Bunge, Job Ndugai akifungua warsha ya wabunge kuhusu vitendo vya unyanyasaji wa watoto wakati wa kuadhimisha Siku ya Watoto Duniani kwenye Ukumbi wa Msekwa, bungeni jijini Dodoma Novemba 202, 2020. Warsha hiyo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Watoto (UNICEF). Kutoka Kulia ni Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson na kutoka kulia ni Mwakilishi wa UNICEF, Shalini Bahuguna na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milisic.
Rose Mweleka (24) ni mfamasia mwenye digrii aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Kampala, Dar es Salaam. Anatumia muda wake kuwafundisha viongozi vijana kusaidia kufanya mabadiliko katika jamii.
Abdulatif Hassan (16), Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chuini Zanzibar ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Zenj FM akielezea jinsi watoto wenye virusi vya UKIMWI wanavyo nyanyapaliwa katika jamii.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai (kulia) , Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson wakiwa katika picha ya pamoja na watoto, vijana waliokuwaq wasemaji wakuu katika warsha hiyo pamoja na viongozi wa UNICEF. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post A Comment: