William Peter Ndilla .

Sumve, Mwanza .

October 15,2020.


Linaweza likaitwa swali jepesi kwa bongo lala, lakini hili sio swali jepesi kabisa katika siasa za sasa za Tanzania. Ningekuuliza wewe kwamba baada ya October 28,2020 utaenda kuishi wapi kwa hakika lingekuwa swali la kijinga kabisa.


Lakini swali hili linakuwa zito hasa anapoulizwa Mgombea Urais wa Chadema Ndugu Tundu Lissu na nashangaa kwanini waaandishi wa habari hawajawahi kumuuliza swali hili ndugu yangu Tundu Lissu.


Katika maisha kuna maswali mawili muhimu ambayo mwanadamu lazima awe ameamua, kwanza katika maisha yako lazima ujue "Utaishi Wapi" na baada ya kifo "Utazikwa Wapi?".


Baada ya kupotea kwa muda mrefu na hata baada ya kupona ndg yangu Tundu Lissu aliendelea kuishi Ulaya yeye na familia yake "Ubelgiji" na baadae akaamua kuizunguka dunia kusaka ushawishi kwa njia "hasi" na akafanikiwa kukutana na akina Amstardam watu ambao hawakuwahi kuijua Tanzania mpaka Tundu Lissu alipoanza kutibiwa Ubeligiji.


BEBERU AMSTARDAM NI NANI?


Huyu ni mhuni mmoja ambaye kaamua kutumia fursa ya kukosa utulivu kwa Lissu kupiga hela za mabeberu.


Huyu hakuwahi kusema lolote kuhusu Tanzania na alianza Kuijua Tanzania baada ya Kupata "deal" la mpango hasi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hii ni ajira kama Ilivyo ajira nyingine!


Baada ya October 28/2020 Mpaka October 31/10/2020 hamtomsikia tena bwana huyu maana kazi yake itakuwa imeisha na wa kumlipa atakuwa hayupo tena.


BILA UCHAGUZI TUNDU ANTIPAS  LISSU ANGERUDI TANZANIA?


Sitaki Kutoa Jibu hapa lakini Kuna Kila dalili Kuwa Tundu Lissu bila Kuwepo Uchaguzi Kwa hakika tungeendelea Kumsikia Kwenye Bomba tu Kwamba Yupo Kwenye Matibabu.


Ajenda Yake Kubwa ya Kurudi Tanzania Ndugu Yangu Tundu Lissu haikuwa Kutafuta Urais Zaidi ya Kuja Kutumia Jukwaa la Uchaguzi Kueneza Chuki na Picha Mbaya dhidi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya CCM.


Ukimsikilza kwa Makini Kwenye Kampeni Zake Muda Mwingi Ndugu Tundu Lissu anatumia Kutoa shutuma "Personal attack" dhidi ya Rais na Kuacha Kuitangaza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Chake.


Hata hivyo Mpango Wake wa Kugombea Ndani ya Chama Umekosa baraka za Uongozi wa Juu Kwani Ilionekana Tundu Lissu hakuandaliwa Ndani ya Chama Chake Zaidi ya Nguvu ya Wafadhili ndio Iliamua Nani awe Mgombea wa Chadema.


Kitengo Cha habari Cha Chadema Wakati huu wa Uchaguzi Kimekufa Kabisa na Bwana Amsterdam ndio amekuwa Mkuu wa Idara ya habari na Uenezi ya Chadema.


Unaweza Ukaona Wazi Kabisa kwamba Kuna Kukosekana Kwa Umoja Ndani ya Chama na Mgombea. Mgombea sio tu kakosa "Support" ya Chama bali pia Kakosa "Support" Mpaka ya Mkewe.


Kwahiyo ni Wazi Kuwa bila Uchaguzi Tundu Lissu asingekuja Tanzania na angeendelea Kusingizia Matibabu Mpaka leo.


JE BAADA YA UCHAGUZI TUNDU ANAELEKEA UBELIGIJI?


Ni Wazi Kabisa Kuwa hivyo ndivyo Itakavyokuwa Kwamba baada ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani October 28,2020 Tundu Lissu tatafanya haya hapa.


Moja,Lissu baada ya Uchaguzi Mkuu atapanda Ndege na Kwenda Ulaya kwa Mabeberu Kuwasilisha Ripoti a.k.a inayoitwa "NIMEONEWA REPORT" akitaja Kufungiwa Kwake na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi.


Ni Wazi Kwamba Kuna "Tundu Lissu Tour" Inakuja tena Kutembelea Ulaya na Marekani Kutafuta Kifuta "Machozi" baada ya Kupigwa na Dkt. John Magufuli "Demonization Plan".


Watanzania twapaswa tuwe tayari Kupokea Kashifa,Matusi,dharau toka kwa Tundu Lissu dhidi ya Tanzania na Mshindi wa Kiti Cha Urais Dkt John Magufuli.


Kinachofuata Kwa Ndugu yangu huyu Itakuwa Pia Kuanda Njia hovu dhidi ya Nchi na ataenda mbali Zaidi Kuvuruga Mipango yetu na Maslahi Yetu ya Nje.


Mabalozi Wetu lazima WAJIANDAE Sana Kujibu Uongo wa Kaka Yangu Tundu Lissu baada ya Uchaguzi Mkuu Kwani bila Kufanya hivyo Maslahi Yetu Machanga Yanaweza Kuharibiwa.


KAMWE TUSIMRUHUSU TUNDU LISSU AKAENDA KUHARIBU MASLAHI YETU KAMA TAIFA NJE YA NCHI.


Kwa Maono Yangu ninaona Kabisa Kuwa Baada ya Kushindwa Uchaguzi October,2020 Ndugu Tundu Lissu anaenda duniani Kusambaza "Propaganda" chafu dhidi ya Tanzania na Mpango huo Utaenda Kuratibiwa na Bwana Amsterdam.


Jamaa huyu anaenda Kujaribu Kwenda Kumchafua Dkt John Magufuli ili Kutimiza Nia Yao Ovu.


Wazalendo wa Nchi hii lazima tujiandae Kuwakabili Jamaa hawa Kwa Njia Zote,hii ni Vita Kubwa Kamwe tusiipuuze.


+255759929244

Mwandishi ni Kada wa CCM na Mzalendo wa Taifa la Tanzania

Share To:

msumbanews

Post A Comment: