Na Mwandishi wetu

Kampuni ya TMS Consultants imewataka  vijana 200 wa vyuo vikuu ambao wamemaliza Shahada ya kwanza na wanategemea kuendelea na mwaka wa pili (Bachelor's Degree) kwa kozi yoyote ile kuhudhuria katika uzinduzi wa program maluum unaotarajiwa kufanyikaKesho October 3 mwaka huu katika hoteli ya Peacock iliyopo mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Sebastian Kingu, amesema kuwa program hiyo imelenga kuwasaidia vijana kwa kupunguza tatizo la ajira rasmi kwa vijana ambapo imekua ni kilio kikubwa nchini Tanzania.

"Tumekusudia kuwasaidia vijana ambao hawapo katika ajira rasmi kwa kushirikiana na washirika wa kimkakati wakiwemo Enterprise Finance (EFL) Madson Property Co.Ltd, Salvation Farm and Marketing Co Ltd,Agricom Africa Ltd pamoja You spices and Green Integration Co.Ltd."amesema Kingu

Amesema kuwa, kila mwaka vijana laki nane (800000) Tanzania huingia kwenye soko la ajira ambapo hii hujumuisha wote waliomaliza vyuo na  wale walio katika vyuo vya ufundi na ujuzi mbalimbali kwani asilimia 5 ndio ambao huingia katika ajira rasmi sawa na vijana (40000) kila mwaka.

Ameongeza kuwa, vijana 760,000 sawa na asilimia 95 huingia kwenye kudi la wasio na ajira rasmi hali inayopelekea wengi wao kuingia katika sekta zisizo rasmi na kusababisha kufanya kazi ambazo hazina tija katika mustakabali wa maisha yao.

Hata hivyo, amesema kiwango cha vijana wasio na ajira tena
wasomi ni kikubwa sana hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa Taifa ikiwemo kutumia madawa ya kulevya, ukahaba na hata kujiunga na mtandao wa kigaidi.

"Hali hii ya ukosefu wa ajira ikiachwa iendelee kukuwa ni mbaya sana kwa nchi yetu kwani vinana wanaweza kutumiwa vibaya na watu wasioitakia mema nchi yetu hata kurubuniwa kuunganishwa katika vitendo vya kigaidi"amesema Sebastian.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: