MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyanjani Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimndai Mgombea Udiwani wa Kata ya Mnyanjani Yakubu Nuru wakati wa mkutano wa kampeni wa Ummy

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na viongozi wa CCM wilaya ya Tanga kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba na Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata ya Mnyanjani Yakub Nuru

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye meza akifuatia matukio mbalimbali kwenye mkutano wake wa kampeni kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkomba na kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata ya Mnyanjani Yakub Nuru
BONDIA Hasani Mwakinyo akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kwenye mkutano huo
MSANII wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akiimba wakati wa kampeni hizo

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akishiriki kucheza kabla ya kunadi sera zake
MSANII mchina mweusi akiimba wakati wa mkutano huo
BONDIA Hassani Mwakinyo kushoto akiwa akimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy MwalimuWananchi wakifuatilia mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu

Wananchi wakifuatilia mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema endapo akichaguliwa atachochea ujenzi wa viwanda vipya katika Jiji la Tanga ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wakina mama ili kukuza uchumi.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyanjani Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni.

Alisema kwamba hilo litafanikiwa kutokana na kuwa na mtandao wa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hivyo ataweka msukumo wao kuja Jijini Tanga kujenga viwanda ili wakina mama waweze kupata ajira na vijana.

Mgombea huyo alisema wakishakuwepo itachangia fursa za ajira huku wajasiriamali wapata biashara,mama lishe ,bodaboda watapata biashara hatua ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi wao na jamii zao

“Lakini jambo la pili ni nitainua uchumi wa Tanga na kusukuma uboreshaji wa Bandari ya Tanga huku akimshukuru Rais Dkt John Magufuli kupawatia Bilioni 372 ili kuboresha Bandari ya Tanga”Alisema

“Hivyo niwaombe wana Mnyanjani mnichague ili nikasukume maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga tuweze kuona meli kubwa zikitia nanga kwenye Bandari ya Tanga”Alisema

 Alisema meli zikitia nanga kwenye Bandari hiyo itasaidia kufungua fursa za ajira kwa wananchi na hivyo kuinua uchumi wa wakazi wa Jiji la Tanga .

“Lakini Bandari ya Tanga ikiboreshwa nitapigania mizigo yote inayoingia nchini na kwenda mikoa ya Kanda ya Kaskazini ishushwe kwenye Bandari ya Tanga badala ya Dar es Salaam”Alisema

 Hata hivyo alisema  ameamua kugombea ubunge ili aweze kuwatumikia wana Tanga sambamba na kuchochea mradi mkubwa wa ujenzi wa bombo la Mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: