NA HERI SHAABAN
Mgombea udiwani wa Kata ya Upanga Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Sulitan Hamed Salim amesema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo itakuwa ya kisasa ndani ya halmashauri ya Ilala.


Sultani aliyasema hayo Dar es Salaam jana,wakati wa kuomba kura kwa wananchi wake ili waweze kumchagua.

" Nitakapochaguliwa
ndani ya  uongozi wangu itaibadilisha kata hii kama Ostebay na kusogeza huduma za kijamii zote ikiwemo mradi wa miundombinu wa kisasa UDMP " alisema Sultan.

Alisema kata hiyo ijajengwa upya chini ya mradi wa UDMP katika kuboresha miundombinu na makazi ya watu .

Sultani aliwataka wakazi wa kata hiyo kumpigia kura mgombea wa nafasi ya urais John Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ili waibuke kwa kishindo waweze kuleta maendeleo katika kuwatumikia wananchi.

Alisema nchi yetu ina maendeleo makubwa sana katika Tanzania ya uchumi wa Viwanda maendeleo yetu yaweze kuja kwa kasi amewataka Watanzania siku ya Octoba 28/2020 kuelekeza kura zao zote za udiwani,ubunge na urais kwa Chama cha Mapinduzi CCM.

Aidha alisema Chama cha Mapinduzi ndio chama kinachotekeleza Ilani ya CCM na yeye kama diwani wa kata hiyo ya Upanga mashariki atatekeleza yote yalioekezwa  katika Ilani hiyo .

Sultan alisema Dunia nzima wanamfahamu Rais wa Tanzania John Magufuli na maendeleo yake yanakuja kwa kasi kutokana na juhudi za Rais Maguguli mpaka nchi ya Kenya wanatamani waongozwe na Rais wa Tanzania kutokana na kuibadirisha nchi mpaka kupanda kufikia uchumi wa kati hivyo watanzania wasifanye makosa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa Raiymond Mwangala alisema Dar es Salaam itakuwa kitovu cha Biashara Serikali tayari imeshamia Dodoma hivyo jiji hili  litakuwa la Biashara litatumika na wafanyabiashara wote wa Afrika na nje ya Afrika katika kununua bidhaa zao na kuzisafirisha .

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa  Raimond alisema ifikapo Octobar 28/2020
ndio itakuwa mwisho wa vyama vya siasa hapa nchini pale mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa John Magufuli atakoibuka kwa kishindo .


Share To:

msumbanews

Post A Comment: