Waziri Mkuu Mstaafu na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema Rais Magufuli anahitaji msaada mkubwa katika kuhakikisha mapambano dhidi ya  rushwa yanafanikiwa.

Waziri Mkuu huyo Mstaafu  amesema hayo leo wakati akifungua kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo amesema enzi za uhai na maisha yote ya baba wa Taifa   alipambana na rushwa, hakupokea wala kutoa rushwa hivyo

Mzee Warioba amesema ajenda ya  Rais John Magufuli ya kulinda rasilimali kwa kupiga vita rushwa ni kazi kubwa na kuwa Rais anahitaji msaada ili kurudisha nidhamu kwa maslahi ya Taifa.

“Rushwa bado ipo kwenye maeneo mbalimbali rushwa  ipo kwenye vyama vya siasa, ipo kwenye vyema vya michezo  na pia rushwa ipo kwenye Taasisi nyingine za serikali.”alisisitiza Warioba

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema  lengo la kongamano ni kuenzi na kujifunza yale yote waliyoyaelekeza Waasisi wa Taifa letu.

Prof. Mwakalila amewaeleza washiriki wa kongamano hilo kuwa mada kuu ni “Mchango wa Mwalimu Nyerere katika Mapambano dhidi ya rushwa” na kusema kuwa mada ya kongamano inagusa makundi yote ya Jamii.

Naye Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Temeke Donasian Kessy amesema rushwa ni zao la uozo wa maadili ambapo humsukuma mtu kufanya jambo la uhalifu, rushwa ni adui wa haki na inatakiwa kupigwa vita kwa vitendo kwa kuwa madhara yake ni makubwa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Mstaafu ludovick Utoh anesema kumekuwa na mazingira tofauti ya utoaji rushwa na kuwa suala la madhara ya rushwa katika Jamii  na Utawala bora yameendelea kustahamili katika nchi nyingi duniani hususan zinazoendelea.

Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO
24.08.2020
Share To:

msumbanews

Post A Comment: