Katika kubabiliana na changamoto kadhaa zinazowakabili wakulima ikiwemo kutotambulika rasmi kwenye taasisi za kifedha, serikali imeanza kutoa vitambulisho maalum kwa ajili yao, hususani wanapohitaji huduma za kifedha.
“Vitambulisho hivyo vya kisasa vitakuwa na ‘chip’ maalumu itakayobeba taarifa zote muhimu kuhusu mkulima hatua ambayo tunaamini itazirahisishia taasisi za fedha mlolongo mrefu wa kukusanya taarifa za wadau hao na hivyo kuwapatia mikopo kwa wakati,’’ alisema Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga baada ya kukabidhi vitambulisho hivyo vya mfano kwa wakulima 15 wa awali katika mkutano mkuu wa wadau wa korosho uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Lindi.
Katika mkutano huo, wadau mbalimbali wa kilimo cha zao la korosho nchini wameonesha kuvutiwa na huduma mpya ya NBC Shambani, huku wakibainisha ujio wa huduma hiyo maalumu kwa ajili ya wakulima utaondoa changamoto za muda mrefu ikiwemo kutopata mikopo kwa wakati sahihi.
“Licha ya uwepo wa huduma nyingi za kibenki kwa ajili ya wakulima bado tumeendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa za huduma za kifedha ikiwemo ucheleweshwaji wa mikopo na tunapoipata inakuwa sio wakati sahihi na hivyo kusababisha wengi wetu kuitumia kwa matumizi yasiyokusudiwa"
"Ni matarajio yetu ujio wa huduma NBC Shambani utatatua changamoto hii na sisi tupo tayari kuipokea,’’ alisema Salum Muhila, mkulima wa korosho kutoka Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
Credit - Azam TV.
Post A Comment: