Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule leo amemkabidhi fomu za Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi, Bw. Singa Maulidi Kalekwa kupitia chama cha Chama Cha Jamaii (CCK)
      Mgombea huyo aliwasili kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi  Jimbo, eneo la Sekei mjira ya  saa 06:00 mchana na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi mnamo saa 06:16 mchana,  akiwa ni mteule wa chama cha Kijamii  - CCK kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
        Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo,  kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B,  kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
        Hata hivyo Msimamizi Mtambule, amemtaka mteule huyo, kuchukua muda kusoma melekezo yanayotolelewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,  kupitia vitini vya maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sambamba na kuheshimu taratibu za uchaguzi kwa kufuata maelekezo hayo kutafanya uchaguzi kuwa wa amani, huru na  haki kwa manufaa ya watanzania wote.
        Mgombea huyo amefanya kufikisha idadi ya Wagombe nane kutoka vyama nane vya siasa, kuchukua fomu ya Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.Share To:

msumbanews

Post A Comment: