Waziri wa Elimu,sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wanaosomba fani mbalimbali katika chuo cha ufundi cha Nyamidaho
 Muonekano wa jengo la utawala katika chuo cha ufundi stadi VETA Nyamidaho

 Mkuu wa kitengo cha ujenzi katika chuo cha ufundi Nyamidaho Salu Mashimo akimpa maelezo waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia baadhi ya vifaa katika idara yake vinavyofanya kazi
 Waziri wa Elimu Professor Joyce Ndalichako akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyamidaho(hawapo pichani)katika hafla ya uzinduzi wa chuo cha mafunzo stadi VETA Nyamidaho Kasulu.
 Waziri wa Elimu,sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akinawa mikono kwaajili ya kujikinga na ugonjwa homa kali ya mapafu(corona)alipowasili katika chuo cha ufundi stadi VETA Nyamidaho kwaajili ya uzinduzi wa chuo hicho.

 Waziri wa Elimu,sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe kukizindua chuo cha ufundi stadi cha VETA Nyamidaho kulia kwake ni mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga na kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Taifa ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA Taifa Peter Maduki.


WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 48 kwaajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika halmashauri ishirini na tisa  nchini nzima lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mkoa unakuwa na vyuo vya ufundi hadi kufikia mwaka 2025.

 Ndalichako ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyamidaho kwenye hafla ya uzinduzi wa chuo cha ufundi stadi Nyamidaho kilichopo Wilayani Kasulu.

Waziri alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2019/20 tayari vyuo 20 katika halmashauri mbalimbali nchini vimeshakamilika huku jitihada za kuongeza vyuo vingine zinaendelea.

Alisema uanzishwaji wa chuo hicho ni mwendezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenda vyuo vya ufundi stadi katika kila Wilaya nchini ili huduma hiyo iwe karibu na wananchi ili vijana waweze kujipatia ujuzi.

Alisema chuo cha Nyamidaho kimetokana na majengo yaliyokuwa yakitumiwa na Taasisi ya World Vision ambapo serikali imekarabati majengo yaliyokuwepo na kujenga mengine.

Ndalichako alisema kuwa jumla ya shilingi milioni 534 zilitolewa kwaajili ya kazi hiyo na mpaka sasa zimetumika milioni 477 hadi kukamilisha ujenzi huo hivyo ameridhia ombi la kiasi kilichobakia kutumika kuanzisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kiume.

Amesema katika mwaka 2019/20 vyuo 10 vya halmashauri vimeshajengwa na tayari vimeanza kutoa mafunzo.

Naye Mkuu wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kukamilisha ujenzi wa chuo hicho pia amewataka wakazi wa kijiji cha Nyamidaho kuhakikisha watoto wao wanajiunga na chuo hicho.

"Vijana wa Mkoa wa Kigoma hasa wanao toka katika kijiji hiki cha Nyamidaho sasa ni jukumu lao kuchangamkia hii fursa ambayo ni mkombozi na itatua changamoto ya ajira kwa vijana pia hata watu wazima wanaoweza kusoma kwa muda mfupi katika fani mbalimbali"alisema

Mwenyekiti wa bodi ya Taifa ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi  VETA Taifa   Peter Maduki aliishukuru serikali kwa kuendelea kuimarisha vyuo vya ufundi nchini,nakusema chuo hicho kipya kilichozinduliwa kina wanafunzi 70 pia ameuagiza uongozi wa VETA kutoa mafunzo ya uwashi bure kwa wanafunzi wanaotoka Nyamidaho.

Alisema chuo cha ufundi VETA cha Nyamidaho kinakuwa ni chuo cha pili cha VETA kwa Mkoa wa Kigoma hivyo wigo umekuwa mpana kwa vijana kusomea mafunzo ya ufundi stadi kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma.
Share To:

Post A Comment: