Na Esther Macha, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya , Albert Chalamila amesema kuwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona wilaya zote zimeagizwa kuwa na kantini ya kuhifadhi watu watakaobainika kuwa na dalili na kwamba tayari serikali mkoani hapa imepokea dawa na vifaa tiba vya kutosha kutoka katika Bohari ya Dawa (MSD).
Chalamila aliyasema hayo jana wakati akipokea vifaa hivyo kutoka Bohari ya Dawa pamoja na kutembelea maeneo ya vituo vya afya yaliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi watu watakaobainika na dalili.
" Kwa sasa Serikali tumejianga kikamilifu katika mipaka yetu ili kuhakikisha raia wote wa kigeni wanaoingia nchini wanapimwa joto na vifaa maalum ili kuweza kudhibiti maambukizi ya corona na kuimarisha ulinzi katika mpaka yetu na kudhibiti njia za kipanya "alisema.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa alisema raia tisa wa kigeni wamehifadhiwa kwenye kantini wakiwa katika uangalizi maalum na kufanyiwa vipimo ndani ya siku 14 ili kubaini kama wanaviashiria vya maambukizi ya ugonjwa wa homa ya corona.
Aidha Chaamila alisema zaidi ya 150 milioni za raia wa wakigeni waliongia nchini kinyume cha sheria zimetaifishwa na Serikali mkoani hapa .
Katika hatua nyingine akiwa katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani Chalamila ameonya vijana kuachana na tabia ya kuboresha mapenzi kwa kunyonyana ulimi na kwamba hiyo ni hatari kubwa inayoweza kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwepo corona.
"Vijana nawaonya acheni tabia hiyo mara moja kwani kuna baadhi yenu bila kupeana ulimi ni kunogesha upendo upendo hata bila kupeana ulimi inawezekana tu shirikianeni na Serikali kupinga corona kwa kuepuka tabia hatarishi "alisema.
Aidha kwa upande mwingine aliwaondoa hofu wafanyabishara kuwa serikali haitoweza kuwafungai katika biashara za kumbi za starehe,mamalishe, na maduka ya pombe na badala yake wafanyabishara wazingatia kanuzi za afya kwa kila mmoja kwa nafasi yake kuwa na maji miminika na sabuni yenye dawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Jiji la Mbeya , James Kasusura ameagiza mabasi yote yanayotoka na kuingia katika vituo vya mabasi kuwa na sabuni yenye dawa na maji tililisha ikiwa ni pamoja na pikipiki za mataili matatau (bajaji) bodaboda na tax.
Alisema hilo ni agizo na lazima litekelezwe na kufanya ufuatiliaji na watakaobainika kutofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa sambamba na kuwataka wananchi kuwafichua ili kuweza kuunga mkono jitihada za serikali kupiga vita ugonjwa wa corona.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya , William Ntinika alisema kuwa jamii imeonyesha mwamko mkubwa wa kujikinga ikiwa ni kwenye migahawa, maduka ya pombe, na kumbi za starehe.
Ntinika alionya wananchi kuachana na dhana ya kuuchukulia ugonjwa huo kama ni wakutisha na kuchangia jamii kujenga hofu na kwamba ufike wakati kutii sheria bila shuruti kwa kutokuwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi ili kukabiliana na changamoto na maambukizi ya corona.

Post A Comment: