Soko la Samunge likiteketea kwa Moto kama lilivyokutwa na kamare ya matukio jijini Arusha usiku wa kuamkia leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati soko la Samunge lilipokuwa linaungua leo jijini Arusha majira ya usiku wa kuamkia leo.


Soko la Samunge likiteketea na Moto usiku wa kuamkia leo jijini Arusha ambapo imeelezwa kuwa thamani ya Mali iliyoteketea bado haijajulikana huku mfanyabiashara Mmoja akifariki kwa mshtuko  Mara baada ya kukuta maduka yake matatu yameungua.
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mtu mmoja amefariki dunia Mara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha baada ya kufika na kushuhudia maduka yake yote yakiwa yameteketea na moto.

Akiongea na waandishi wa habari Sokoni hapo Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita amethibitishakea kwa tukio hilo huku akibainisha kuwa hadi Sasa thamani ya Mali zilizo teketea haijajulikana


Aidha wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu  mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake 

Kaimu kamanda Koka  alieleza kuwa majira ya saa 23:30hrs, katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana uliwaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo ambavyo idadi na thamani yake bado haijajulikana. 
Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu. 
 vimeungua.

Mtu huyo alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospital ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu. 
Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo. 

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari. 
Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona majanga kama haya ya moto kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kudhibiti matukio kwa haraka kabla ya kuleta madhara makubwa. 

 Alitoa wito kwa wananchi na kuwaomba  pamoja na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vikifanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tukio hilo

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: