TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ijulikanayo kama elimu kwa vijana kupitia michezo (YES TZ) imepokea msaada wa Ruzuku ya Dolla za kimarekani 42,000 sawa na sh. Mil.97,012,986.775 kwa ajili ya matumizi ya kuijengea taasisi uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kusaidia serikali kufikia malengo yake mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ,Kenneth Simbaya alisema Ruzuku hiyo imetolewa kutoka Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA) na kwamba fedha hizo zitatumika kuanzia January 2020 mpaka June 30,2021.
Alisema kupitia waelimishaji rika wa kujitolea wa taasisi hiyo kumekuwa na ongozeko kubwa la vijana ambao wamepata mafunzo toka kwa vijana wenzao wanaojitolea.
Aidha Simbaya alisema waelimishaji rika hao wameweza kupeleka elimu sahihi kwa vijasna wenzao ambayo imekuwa msaada mkubwa.
Alisema kuwa vijana 4000 walifikiwa na vijana wa kujitolea na wengi wao ni wanawake kutoka kata tisa(9).
Kwa upande wake Mwelimishaji rika wa kujitolea ,Katie Dunbar alisema kuwa kujitolea kuna faida kubwa sana kwa vijana kwani wanajifunza vitu vingi sana na kupata uzoefu wa kufanya kazi.
“Mfani mimi mwenyewe hapa nimejinza vitu vingi kwa kujitolea ukiachilia mbali kupata uzoefu wa kujitolea kufanya kazi kumeniwezesha kukuza mtandao wa watu ninao wafahamu ambao ni muhimu katika maisha yaqngu ya kikazi pamoja na kuongeza marafiki”alisema Dunbar.
Post A Comment: