Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akitoa tamko la kuwatumbua maofisa wa NIDA mkoa wa Ruvuma 


 WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola  amewatengua madaraka maafisa wawili wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) wa mkoani Ruvuma kwa kosa la kutogawa namba za utamburisho wa NIDA kwa wananchi .Mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvuma

 Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Songea mkoani humo amesema kuwa amewatengua vyeo maafisa wawili akiwemo Afisa wa NIDA mkoa wa Ruvuma  Seifu Mgonja pamoja na afisa wa Wilaya ya Tunduru.

 Waziri Lugola aliyekuwa kwenye ziara ya siku moja mkoani humo alisema kuwa maafisa hao wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Serikali la kuwataka waweze kuwakamilishia wananchi usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa wakati.

 Akiyataja baadhi ya makosa kwa maafisa hao alisema kuwa afisa wa mkoa  amekaa na namba za vitamburisho vya Wananchi zaidi ya 14,000, bila kuwapelekea taarifa ili wananchi hao waweze kupata fursa ya kusajili laini zao  ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika Januari 20 mwaka huu.

  Kwa upande wa afisa wa Wilaya ya Tunduru ambaye hakumtaja jina  Waziri huyo amesema kuwa amekaidi wito wa kumtaka aweze kufika kwenye ziara yake ili wapeane taarifa pamoja na kuzitatua changamoto zinazowakabili katika zoezi hilo.

  “Siwezi kukubali upuuzi huu ni lazima watu tukipeana kazi tuzitekeleze kwa manufaa ya wananchi na Taifa, hivyo hao maafisa vyeo vyao nimevitengua kuanzia sasa “amesema Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola.

  “Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt,John Pombe Maguli inawajali wanyonge hivyo mimi nikiwa Waziri wa Mambo ya Ndani nitapambana na watu wanaokwamisha jitihada za Serikali”amesema Lugola.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka askari polisi kufanya kazi zao kwa weredi, kwa kutenda haki pale wanapofanya kazi za wananchi hasa wanapohitaji huduma kwenye ofisi hizo.

 Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya Askari kuwabambikia kesi watu ,Kuwanyima dhamana bila sababu za msingi,Kuwabambikia makosa wamiliki wa vyombo vya moto ambayo hata hayastahili kwa lengo la kujinufaisha.

                   
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: