Na Ferdinand Shayo,Arusha

Serikali imejipanga kuhakikisha inakuza sekta ya Uvuvi nchini kupambana na upungufu wa mazao ya samaki ambapo sasa zinazalishwa tani 350,000 huku mahitaji yakiwa tani 700,000

Akitoa taarifa kwenye banda la wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonyesho ya Nanenane kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha ambapo imeonekana kuwepo changamoto kubwa hivyo juhudi zinahitajika kufikia lengo la ongezeko la mazao ya samaki.

Nae Mtaalamu wa sekta ya mifugo na Uvuvi Fredrick Francesis amesema kuwa mwananchi anahitajika kula kilo 20 za samaki kwa mwaka ambapo uzalishaji upo chini ya mahitaji hivyo serikali imeandaa mikakati ya kukuza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji na kuwa na ziada kwa kuacha kutegemea samaki wa maji halisi na kuzalisha kwenye mabwawa.

Kwa upande wake Jackson Samson kutoka kampuni ya Aqua fish com amesema kuwa ufugaji wa samaki hauhitaji fedha nyingi sana kuanza kwani mtaji wake hauzidi kiasi cha 50,000 hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili kuongeza uzalishaji wa samaki.

Afisa  uvuvi wilaya ya Mwanga Said Msemo amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya uvuvi haramu hivyo kuwataka wafanyabiashara wa samaki kutovua samaki wasiofikia viwango vilivyowekwa na serikali si chini ya futi 3
Share To:

msumbanews

Post A Comment: