Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mkurugenzi mtendaji wa EMEA Bw. Helmut Butterweck wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.


Waziri Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa kutoka Wizara ya Afya wakiongea na moja kati ya watu waliojitokeza kuchangia damu, katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.


Baadhi ya picha za Kikundi cha Wasanii wa filamu Tanzania wakionesha igizo kuhusu uhamasishaji kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu, tukio limefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.


Jopo la watu waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha, yaliyofunguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


Mashine kubwa zenye gharama inayokadiriwa kuwa dola za kimarekani 600,000 (laki sita) kila moja ambayo ni sawa fedha za Kitanzania bilioni 1.4, zilizozinduliwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: