Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa James Mdoe ameongoza ujumbe  wa Tanzania kwenye mkutano Mkuu wa 62 wa kimataifa wa kuendeleza matumizi salama ya nguvu za nyuklia unaofanyika mjini Vienna nchini Austria.

Akizungumza katika mkutano huo mjini Vienna  Profesa Mdoe ameishukuru  IAEA kwa kuisaidia nchi ya Tanzania mashine ya kuchunguza na kutibu saratani ambayo inatumika katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza na  misaada ya kiufundi katika hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es salama pamoja na  misaada ya kuwasomesha  wataalam kwenye eneo la Teknolojia  ya nguvu za nyuklia.

Profesa Mdoe pia amekieleza kikao hicho Cha kimataifa kuwa nchi ya Tanzania iko  tayari   kushirikiana na IAEA katika kuendeleza matumizi salama ya nguvu ya nyuklia.

Balozi wa kudumu kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva nchini Uswis James Msekele naye anashiriki mkutano huo.

Mkutano huo ulioanza Septemba 17 utahitimishwa Septemba 21, 2018 huko mjini Vienna nchini Austria.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
19/9/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: