Klabu ya soka ya Simba imemtangaza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi wa siku ya ‘Simba Day’  ambapo timu hiyo itashuka uwanja wa taifa kuwakabili  Asante Kotoko ya Ghana Agosti 8, 2018.
                                                                                                                                                         Afisa habari wa Simba, Haji Manara amethibitisha hilo mbele ya waandishi wa habari kuwa tayari Waziri mkuu Majaliwa atakuwa mgeni rasmi siku hiyo.
”Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekubali ombi letu, na ninaomba nitangaze rasmi kuwa yeye ndio atakuwa mgeni rasmi kwenye tamasha letu la ‘Simba Day’ akiongoza shughuli zote ambazo zitafanyika siku hiyo,”- amesema Manara.
Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kutojihusisha na masuala ya kugushi tiketi kwani wao kama klabu wamejidhatiti kuhakikisha watu wa aina hiyo hawapati mwanya ndio maana suala la usimamizi wa tiketi uwanjani wamelikabidhi kwa Suma JKT.
Mabingwa hao wapya wa ligi kuu huadhimisha siku hiyo ya Simba Day kila ifikapo Agosti 8 ya kila mwaka kwa kufanya shukhuli mbalimbali za kijamii na kuwatambulisha wachezaji wao wapya.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: