Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Msanii Johmakini kutoka kundi la Weusi atapanda jukwaani katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani itakayofanyika Agust 12 katika Chuo cha Walimu Patandi ambapo vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini watahudhuria katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yanafanyika Arusha na kudhaminiwa na shirika lisilokua la kiserikali la DSW.

Johmakini ambaye anafanya vizuri katika Muziki wa Hip Hop na kukubalika na makundi ya Vijana na wenye umri wa makamu kutokana na uwezo wake mkubwa wa mashairi  atawaburudisha vijana kwa ngoma zake zinazotakamba ukiwemo wimbo wake Wa Mipaka,stimu zimelipiwa,I see me ,Don Bother na nyingine nyingi.

Tayari Johmakini amewasili jijiji Arusha na anatarajia kuperform live huko Patandi siku ya kesho huku umati mkubwa wa vijana ukitarajia kumshuhudia msanii huyo anayefanya vizuri Tanzania,Afrika Mashariki na kati.

Johmakini amesema kuwa siku ya kesho atafanya show ya aina yake ambayo haijawahi kutokea hasa ukizingatia kuwa katika Mkoa wa Arusha ana mashabiki wengi wanaomkubali na kuunga mkono kazi zake.

“Nitapata fursa ya kuimba nyimbo zangu na vijana tungo zangu zimekua zikiwaelimisha vijana wengi na huo ndo mchango wangu kwa vijana wa Kitanzania “ Anaeleza Johmakini

Afisa Habari Shirika lisilokua la kiserikali la DSW Philomena Marijani  ambao ndio wadhamini wakubwa wa maadhimisho hayo wamesema kuwa wamemchagua msanii Johmakini kwa kuwa vijana wengi wanamsikiliza hivyo ana nafasi kubwa ya kuhamasisha maendeleo na kuwaelimisha vijana kupitia tungo zake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: