Haya yamebainishwa katika hafla ya makabidhiano ya hundi ya shilingi 200,000,000 kwa vikundi 52 vya wajasirimari 52 na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeo wilayani Nyamagana.
Mhe. Mhandisi Kabeo amekabidhi hundi ya fedha hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi kuelekeza kila halmashauri kwa kuzingatia sheria na kanuni inayoelekeza 10% ya mapato ya ndani kwa kuwawezasha kimtaji wajasirimali kupitia mfuko wa Vijana na wanawake pamoja na walemavu. Vikundi vilivyokabidhiwa fedha itaviwezesha kukuza mtaji, kuongeza thamani ya bidhaa, kutoka kwenye uchuuzi na kufikia uwekezaji pamoja na upanuzi wa soko la kibiashara. Hivyo Mhandisi Kabeo amewasa wajasirimali kutumia fursa hiyo vyema na weredi kwa kuzingatia jedwari la marejesho ili fedha hiyo iweze kusaidia vikundi vingine.
Naye Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula amesema wamezidi kuisimamia serikali kupitia halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuhakikisha inatenga mapato yake ya 10% ili kuwawezesha Wajasirimali kulingana na Sera ya Chama Cha Mapinduzi inayoelekeza makato ya 10% ambapo ni 5% kwa Vijana na 5% kwa wanawake pasipo kuwatenga walemavu.
Kwa mwaka 2018/2019 wajasirimali wanatarajiwa kunufaika na tengo la 10% ya mapato ya halmashauri ya Jiji la Mwanza katika mfuko wa maendeleo ya Wanawake na Vijana kwa makisiao ya jumla ya shilingi 1,400,000,000.00 ambapo fedha hizi zitakuwa zinatolewa kwa awamu ikiwa katika awamu hii Mwenge wa Uhuru umekabidhi 200,000,000.00. Ili kukuza mitaji katika uongezaji wa thamani ya bidhaa, elimu ya ujasirimali na masoko na biashara ili kutoka dhana ya uchuuzi na kufikia uwekezaji ambao ni mwelekeo wa dhana ya uchumi wa viwanda.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: