Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo amesema miongoni mwa matatizo ambayo watumishi wengi wanaostaafu au kuondolewa katika nafasi wanazoteuliwa na Rais ni kukiuka kiapo chao cha kutunza siri.
Dk. Dialo alisema wapo watumishi wengi hususan wa kuteuliwa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala na wengine wamekuwa wakitoa siri walizopata wakati wakitumikia nafasi zao kitendo ambacho kinakiuka kiapo chake.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni alipozungumza na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mwanza walioteuliwa Julai 28, mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli huku akiwataka waliostaafu kwa umri na walioondolewa katika nafasi zao kuendelea kutunza siri za Serikali.Mke
Post A Comment: