Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imebaini wafanyabiashara wa utalii wa kujitegemea zaidi ya 500 maarufu kama freelancer wasiokuwepo kwenye mfumo wa ulipaji kodi katika kipindi cha siku 10 ilizofanya ukaguzi katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro jijini Arusha.

Kwa kutokuwepo kwenye mfumo rasmi wa wafanyabiashara hawa inasababishia serikali kukosa mapato ambayo yangetokana na kodi ya mapato kutoka kwa wafanyabiashara hao na hivyo TRA imebaini hilo baada ya kufanya ukaguzi wa hali ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wa utalii na hivyo TRA  imewataka kuwasilisha nakala za mikataba yao ya kazi wanazofanya ili mamlaka iweze kufuatilia mienendo ya biashara zao na kuwakadiria kodi stahiki kama wenzao wenye leseni za kufanya biashara hizo.

Akizungumza baada ya kufanya operesheni ya kukagua hali za ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya utalii na kuwaingiza watalii kupitia geti la Mamlaka ya Ngorongoro Kamishna wa Kodi za ndani wa TRA, Bw.Elijah Mwandumbya amesema kuanzia sasa wafanyabiashara wa utalii watatakiwa kuwasilisha mikataba yao ya kazi ili serikali iweze kuwakadiria kodi na kukusanya kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi za nchi.

“Serikali kupitia TRA na wadau wengine wa utalii nchini imejipanga kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inakua na mchango mkubwa katika taifa ili serikali ipate fedha za kuendesha miradi ya maendeleo ambayo yatanufaisha watanzania wengi”, amesema Bw. Mwandumbya.

Naye msimamizi wa zoezi hilo kutoka TRA Bw. Emmanuel Marcel amesema kuwa wafanyabiashara wanaojitegemea ambao hawajajisajili popote, inakuwa ngumu kuwafuatilia kwa kuwa wanatumia miundo mbinu ya wenzao waliosajiliwa  na kutumia mwanya huo kukwepa kodi.

“Wengi wao wanaingiza magari yao kwenye kampuni zilizosajiliwa na wao wanakuwa hawaonekani kwenye mfumo na hivyo kutokuwa kwenye mfumo wa kulipa kodi, lakini kwa mkakati huu tuna uhakika watakuja kwenye mfumo na watalipa kodi”, amesema Bw. Marcel

Kwa upande wao waongoza watalii Paul Kasmir wamesema kuwa kuwepo kwa mikataba itakayowasilishwa TRA itasaidia serikali kupata mapato pamoja na kulinda maslahi ya waongoza watalii.

Alisema kuwa zoezi hilo limefanyika bila kusababisha usumbufu kwa watalii jambo ambalo linapaswa kuigwa na taasisi nyingine.

Tanzania inakadiriwa kuwa na wafanyabiashara ya utalii 2200 ,Wafanyabiashara walioko kanda ya kaskazini ni 1403 huku Wafanyabiashara wanaojitegemea wasiotambulika ni zaidi ya 500 katika siku 20 walizofanya ukaguzi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: