Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula  ameshukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa awamu ya tanu wa Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kujenga daraja la  Kanindo Sawah litakalo gharimu shilingi 189,000,000.


Mhe Mabula amebainisha hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Kata ya Kishiri. "Nina farajika sanaa ahadi niliyowaahidi Wananchi katika kunadi Ilani ya uchaguzi wa 2015-2020 inatekerezeka kwa vitendo, sasa hatuzungumzi habari za tutajenga bali tunajenga" Alisema.  Amewasihi walaka wa barabara Mjini na Vijijini TARURA kukamilisha ujenzi huo ndani ya mkataba wake wa miezi mitano ili kuwezesha kufungua barabara hiyo inayoziunganisha Kata nne ili kuondoa msongamano wa magari mjini.

Ukamilishaji wa ujenzi wa daraja hili utatumia miezi mitano chini ya usimamizi wa  TARURA  unakudiwa kuunganisha Kata nne ikiwa ni Kata za  Kishiri, Igoma, Lwanhima pamoja na Buhongwa.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: