Baada ya agizo la serikali la kujenga maabara za masomo ya Sayansi katika shule zote za sekondari, maabara hizo zimeanza kuzaa matunda kwa kuwa na ongezeko la wanafunzi katika maso ya Sayansi pamoja na ongezeko la ufaulu pia.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Shule ya sekondari Osiligi kata ya Olturumet moja ya shule iliyopata maabara baada ya agizo la serikali, maabara hiyo imewezesha ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi katika masomo hayo kulinganisha na miaka ya nyuma kabla ya uwepo wa maabara.
Hayo yamethibitishwa na mkuu wa shule  ya sekondari Osiligi, mwalimu Rosemary Tiganyira alipozungunza na mwandishi wa habari hizi alipotembelea shule hapo.
Mkuu huyo wa shule amesema kuwa, tangu kujengwa maabara ya masomo ya Sayansi mwaka 2016, wanafunzi wameanza kufanya vizuri katika masomo hayo tofauti  na hapo awali kulipokuwa hakuna maabara.
Mwalimu Tiganyira, ameongeza kuwa  licha ya kuwa na wanafunzi wachache wanaochagua masomo ya sayansi na kuwa na walimu wachache lakini bado wanafunzi wanaonesha kufanya vizuri tofauti na masomo ya Sanaa yenye walimu wengi.
Amesema kuwa kwa matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ya mwaka 2017, wanafunzi  47 waliofanya mtihani wa Biolojia, walifaulu wote kwa alama A mpaka D, wanafunzi 14 kati ya 18, walifaulu somo la Kemia na wanafunzi 7 kati ya 18 nao walifaulu somo la Fizikia kwa alama A mpaka D.
Hata hivyo mkuu huyo wa shule amethibitisha kuwa, wanategemea wanafunzi wa kidato cha nne watakaofanya mtihani mwaka huu kupata matokeo mazuri zaidi hasa wakiangalia matokeo ya mitihani ya ndani.
" Wanafunzi kwa sasa wanafurahia masomo ya Sayansi na wanafanya vizuri, tunategemea kiwango cha ufaulu kuongezeka kwa kuwa, hata mayokeo ya mitihani ya ndani, wanafunzi wanafanya vizuri" amesema mkuu huyo wa shule
Naye Meshaki Saruni mwanafunzi wa kidato cha nne amesema kuwa, uwepo wa maabara unawasaidia kulipenda somo, kujiamini kwa kile wanachokifanya na zaidi vitendo vinawawezesha kukumbuka kile walichojifunza.
Ninapofundishwa darasani, nikaenda maabara kufanya practical na kuthibitisha kile nilichokisoma, inanifanya kulipenda sana somo, kuamini kile nilichojifunza na sio rahisi kusahau, tofauti na kujifunza bila practical" amesema Meshaki.
Mwanafunzi Meshaki amewataka wanafunzi kutokuogopa masomo ya Sayansi  kwa kuyaona ni magumu na kuwaondoa wasiwasi kuwa kama kuna maabara, masomo ya Sayansi ni marahisi mno.
Licha ya wanafunzi hao kuanza kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi lakini bado kuna changamoto ya upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi.
Halmashauri ya Arusha inaendelea kukamilisha ujenzi wa maabara kwenye shule 27 za serikali huku ikiwa na jumla ya vyumba 74 vya maabara za masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia huku ikiwa na upungufu wa vyumba 7 vya maabara.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: