Rais John Magufuli leo mchana Aprili 2,2018 anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo wa rada za kuongoza ndege.
Mfumo
 huo wa rada za kuongozea ndege unajengwa katika vituo vinne vya Uwanja 
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA); Uwanja wa Ndege wa 
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA); Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza 
na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
Ujenzi
 unafanywa na Kampuni ya M/S Thales Las France SAS ya nchini Ufaransa 
ukigharimu Sh67.3 bilioni fedha zinazotolewa na Serikali ya Tanzania kwa
 asilimia 100.
Mkurugenzi
 Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari 
amesema leo Jumatatu Aprili 2,2018 kuwa ujenzi utakamilika ndani ya 
miezi 18.
Amesema mradi huo utasaidia kurahisisha huduma za utafutaji na uokoaji kunapotokea ajali za ndege.
Johari
 amesema pia utaiwezesha nchi kukidhi viwango na miongozo ya Shirika la 
Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na kujenga imani ya watumiaji wa 
anga ya Tanzania.
Tayari wageni wamewasili eneo la uzinduzi wakiwamo mawaziri, wabunge, mabalozi na wananchi.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasili akiongozana na msanii 
wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu Diamond.
Post A Comment: