Kiungo
wa kati wa Barcelona Andres Iniesta, 33, ataeleka katika klabu ya China
mwisho wa msimu huu huku chupa bilioni mbili za mvinyo zikiorodheshwa
katika makubaliano hayo.. (Marca - in Spanish)
Liverpool
haina fursa ya kumsajili kipa wa Roma na Brazil Alisson, 25, mwisho wa
msimu huu kulingana na rais wa klabu hiyo James Pallotta. (Sky Sports)
Mkufunzi
wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumwacha kiungo wa kati
aliyenunuliwa kwa kitita cha £89m Paul Pogba, 25, kuondoka klabu hiyo
pamoja na mshambuliaji Anthony Martial, 22, beki wa Uholanzi Daley
Blind, 28, huku beki wa Itali Matteo Darmian akitarajiwa kuuzwa. (Mail)
Darmian, 28, anasema kuwa atafanya uamuzi kuhusu ombi la uhamisho wake kutoka klabu ya Seria A Juventus mara moja. (Express)
Manchester
City itampatia meneja Pep Guardiola kitita cha £200m za uhamisho baada
ya kushinda taji la ligi , huku kiungo wa kati wa Napoli na Italy
Jorginho, 26, pamoja na kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk ,24, raia wa
Brazil Fred wakilengwa. (Mirror)
Mkufunzi
wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuanzisha tena mpango wake wa
kutaka kiungo wa kati wa Napoli Piotr Zielenski. Klabu hiyo ya Itali
iliishinda Liverpool kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa mika
23 2016.(Sun)
Trent
Alexander-Arnold, 19, amesaini kandarasi ya muda mrefu na klabu yake ya
Liverpool huku akitarajia mshahara wake kuongezeka maradufu.. (Mirror)
Manchester
United wametuma maskauti kumtazama kiungo wa kati wa Lazio na Serbia
Sergej Milinkovic-Savic, 23, huku mkufunzi Jose Mourinho akitaka
kuwasajili viungo wa kati wawili mwisho wa msimu.. (Mail)
Mshambuliaji
wa Man United na Uingereza Marcus Rashford, 20, yuko tayari
kuchelewesha kandarasi mpya na klabu hiyo baada ya kupuuzwa katika
kikosi cha kwanza. (Sun)
Mkufunzi
wa Arsenal Arsene Wenger amekosoa hatua ya ligi ya Uingereza
kuchelewesha matumizi ya mbinu ya VAR katika mechi.. (Times)
Tottenham
iko tayari kumuuza kiungo wake wa kati Mousa Dembele, 30, na tayari
wamepata wachezaji wawili wanaoweza kuchukua mahala pake.. (Mirror)
Mshambuliaji
wa Atletico Madrid Fernando Torres, 34, anatarajiwa kuipuuza ligi ya
kwanza ya China na badala yake kuelekea ligi ya Marekani ya MLS baada ya
kutangaza kwamba ataondoka Uhispania mwisho wa msimu huu.. (Marca)
Klabu
ya Boca Juniors inataka kumsajili kipa wa Juventus na Italy Gianluigi
Buffon, 40, na wanamtaka mchezaji mwenza wa zamani na mshambuliaji wa
Argentina Carlos Tevez, kuwasaidia kumsajili. (Radio Continental via
Mail)
Kiungo
wa kati Ruben Loftus-Cheek, 22, bado hajaamua kuhusu hatma yake katika
klabu ya Chelsea baada ya kuonyesha mchezo mzuri alipokuwa katika klabu
ya Crystal Palace kwa mkopo . (Independent)
Kiungo
wa kati wa zamani wa Liverpool na Fulham Danny Murphy anasema kuwa
mkufunzi wa Newcastle Rafa Benitez anaweza kuwa kocha mzuri anayeweza
kumrithi Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal. (Talksport)
Mkufunzi
wa Southampton Mark Hughes anasema kuwa wachezaji wake lazima wafanye
kazi ya ziada iwapo wanataka kuepuka kushushwa daraja.. (Guardian)
Klabu
ya Wolves inataka kutumia £20m kuwasaini kwa mkopo wachezaji Benik
Afobe, 25, na Willy Boly, 27 - kutoka Bournemouth na Porto mtawalia -
kufuatia kupanda ngazi katika ligi ya Premia (Telegraph)
Winga
wa Fulham Ryan Sessegnon, 17,anasema kuwa anataka kucheza katika ligi
ya Premia licha ya klabu chungu nzima kuwasilisha maombi yao. . (Evening
Standard)
Kutoka BBC
Post A Comment: