Wakati Young Africans SC ikielekea kwenye mchezo wake wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya timu ya Welayta Dicha hapo kesho siku ya Jumatano Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa  amesema kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mechi na wanajua matokeo kama watapata matokeo mazuri  wataelekea kwenye hatua ya makundi licha ya kuwa lolote linaweza kutokea.

“Wachezaji wanafahamu umuhimu wa mechi na wanajua matokeo yake wakipata matokeo mazuri  wataelekea kwenye hatua ya makundi, na wao pia wapo kwenye matarajio hayo kama unavyojua mpira hautabiriki sana kama unakumbuka Barcelona walishinda kwake tatu lakini wenzao waliyarudisha na kisha wakatoka kwahiyo lolote linaweza kutokezea kwahiyo wachezaji wangu wanatahadhari kubwa kwakuamini mechi itakuwa ngumu lakini wanamatumaini makubwa kwafaida ya Watanzania wote.”

Mkwasa ameongeza kuwa “Tumewafatilia Welayta Dicha FC wakiwa nyumbani wapoje tunajua mpira wa Ethiopia na mashabiki wanajulikana wenzetu wanakuwa na umoja sana wanapokuwa nyumbani tofauti na sisi huku tunajua tutakutana na hilo pia na sisi wapo wenzetu ambao wameshakwenda huko kusapoti vijana.”

“Matarajio ni kusonga mbele kama unavyojua unapokuwa unacheza Ligi ili kupata wawakilishi kwahiyo sisi ni wawakilishi kwahiyo mechi yetu hii ni kama tupo kwenye kipindi cha pili maana cha kwanza tumeshaongoza kwa bao 2 – 0 kwahiyo tunachotakiwa ni kuongeza moja au kulinda ushindi wetu.”

Kwenye mchezo wa awali uliyopigwa jijini Dar es salaam mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Welayta Dicha magoli yaliyofungwa na Raphael Daudi sekunde 30 tu tangu mpira kuwanza na Emmanuel Martin aliepachika dakika ya 54 ya kipindi cha pili.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: