Mabingwa wa soka nchini timu ya Yanga imethibitisha kupokea mwaliko wa kushiriki michuano ya Kombe la SportPesa kwa mwaka 2018.

Yanga imetoa taarifa hiyo leo huku ikiweka wazi kuwa wapo tayari kushiriki michuano hiyo ambayo mwaka huu itafanyika nchini Kenya baada ya mwaka jana kufanyika hapa nchini.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 4 hadi Juni 10 mwaka huu jijini Nairobi Kenya. Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Bw. Abbas Tarimba amesema timu zingine kutoka Tanzania zitatangazwa ndani ya wiki hii pamoja na utaratibu mwingine utawekwa wazi.

Msimu uliopita klabu ya Gor Mahia ya Kenya ilitwaa ubingwa baada ya kuwafunga ndugu zao FC Leopards mabao 3-0 kwenye fainali iliyopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: