Umoja wa Vijana ( Uvccm ) mkoa wa Arusha umemtunuku hati maalum ya Pongezi Mkuu wa Mkoa Mrisho Mashaka Gambo baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake katika kushuhulika na shida za vijana katika Mkoa wa Arusha.

Gambo alikabidhiwa hati hiyo jana wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr.Mwigulu Nchemba akiwakabidhi kadi zaidi ya vijana 70 waliokwisha kamilisha marejesho ya pikipiki walizokabidhiwa na Mkuu wa mkoa mwaka juzi Dec 11, 2016 kwa masharti nafuu yasiyokuwa na riba.

Akizungumza na Msumbanews Blog Katibu Hamasa wa Umoja wa Vijana Ndg. Omary Lumato alisema

"Sisi kama umoja wa vijana wa cmm Mkoa wa Arusha tumeamua kumpongeza sana Mkuu wa Mkoa kwa kuonyesha juhudi za kuwajali vijana na jitihada za kuwa sapoti katika kuwapatia vitega uchumi vitakavyoweza kuwaondoa vijana katika vishawishi na kushiriki katika vitendo viovu napia tunawasihi vijana wa mkoa wa Arusha kuhakikisha wanatumia hizo pikipiki katika kujikimu kiuchumi na kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya Tano na pia wasikubali kutumika na wanasiasa wanao washawishi kushiriki katika maandamano kwani siasa za maandamano zimepitwa na wakati sasa hivi ni KAZI tu"

Share To:

msumbanews

Post A Comment: