Watu wasiojulikana wamemnyonga hadi kufa Salome Paschal (30) mkazi wa Kijiji cha Zunzuli katika Kitongoji cha Kituli, Kata ya Salawe wilayani Shinyanga na kisha kuutupa mwili wake kwenye kichaka.
Akizungumza jana Jumapili Machi 18, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kwa aliyehusika na mauaji ya hayo.
Akisimulia tukio hilo, mume wa Salome aitwaye Isaya Mshomari amesema mkewe ameuawa Machi 17, 2018 saa nane mchana kwa maelezo kuwa alimuaga kuwa anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani kisha aje awapikie wafanyakazi waliokuwa shambani.
Post A Comment: