Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa mwanafunzi Shija wa Chuo cha Biashara CBE Dar es salaam amefariki kutokana na ugomvi wa mapenzi na ikadaiwa kuwa alirushwa kutoka gorofani kwenye Hostel baada ya kutokea ugomvi huo.

Mkuu wa Chuo hicho Profesa Emmanuel Mjema ambaye ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea katika hosteli binafsi maeneo ya Ilala na sio katika hosteli ya chuo kama ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii.

Profesa Mjema ameeleza kuwa Marehemu anayetambulika kwa jina la Shija alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake na siku ya tukio alikwenda kumtembelea na kumkuta akiwa na Mwanaume mwingine.

Baada ya kuwakuta ugomvi uliibuka na kupelekea Shija kujirusha mwenyewe kutoka ghorofani na kufikwa na mauti.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: