Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limesema kuwa limefungua Jalada la Uchunguzi ili kubaini kama ni kweli Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo alikuwa ametekwa, au alitoa taarifa za uongo.

Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”, ambapo amepatikana akiwa ametupwa barabarani Mafinga mkoani Iringa na baada ya kuzinduka, imeelezwa alijikokota na kuelekea Kituo cha Polisi Mafinga kuripoti

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema, Nondo amepatikana akiwa salama bila jelaha lolote wala kupigwa lakini wamefungua jalada hilo kwa ajili ya uchunguzi na mpaka sasa bado yupo kituoni hapo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: