WATU 28, wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia Chadema (ChADEMA), wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukusanyika isivyo halali.

Mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, watuhumiwa hao wote wanadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa halali kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashtaka wakili wa Serikali, Faraji Nguka leo akisoma mashtaka amedai, lengo la mkusanyiko huo wakiwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kuhusika kwenye tukio hilo na baadhi yao wameweza kutimiza mashati ya dhamana ambayo yamewataka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atayesaini bondi ya shilingi milioni moja na nusu.

 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machine 8, mwaka huu.

Baadhi ya majina ya watuhumiwa hao ni, Tabitha Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mnombo, Abdallah Hamisi, Hussein Kidela, Paulo Kimaro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edina Kimaro.

Wengine ni Fatuma Ramadhani, Asha Kileta, Salha Ngondo, Ally Rajabu, Raphael Mwaipopo, na Athumani Mkawa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: