Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake Emmanuel Masonga wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya leo Februari 26, 2018 baada ya kukutwa na hatia kutumia lugha ya fedhea dhidi ya Rais Magufuli.
Baada ya kuhukumiwa kwenda jela baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wamefunguka yao ya moyoni kuhusu tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.
"Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini 'stay strong' Jongwe" aliandika Niki wa Pili 
Kwa upande wake msanii Rama Dee yeye amesema kuwa ameumizwa sana na bahari ya Sugu kufungwa jela miezi mitano na kudai si picha nzuri katika nchi yetu kwa mambo kama haya. 
"Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri" Rama Dee 
Aidha msanii Izzo Bizness ambaye anaiwakilisha Mbeya vizuri katika muziki wa Hip hop pia ameonyesha hisia zake na kumtaka Mbunge huyo kuwa mvumilivu na kusimama imara katika kipindi hiki.
Mbali na huyo Rapa Roma Mkatoliki alikuwa na haya ya kusema juu ya kifungo cha Sugu "Hata hili lipatita' stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28
Share To:

msumbanews

Post A Comment: