Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ametuma ujumbe kwa watanzania na kuwasihi wasiogope bali waendelee kupaza sauti.
Mbunge huyo ametoa ujumbe wake huo kupitia Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Prof Jay) ambaye yupo mkoani Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mbunge huyo ambaye anatuhumiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye mkutano wa hadhara.
Katika kesi hiyo inayoendelea leo asubuhi mkoani Mbeya anategemewa RCO na RPC wa Mbeya kusimama kutoa ushahidi wao leo.
Sugu pamoja Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya.
Viongozi wote hao wawili walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Januari 16 na kupelekwa mahabusu siku hiyo hiyo , baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.
Sugu kwa sasa anawakilishwa mahakamani na Wakili Peter Kibatala baada ya Mawakili wake wa awali kujivua.
Post A Comment: