Klabu ya soka ya Manchester United leo Jumapili Februari 11, 2018 imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini kutoka kwa klabu ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka England.

Goli la Newcastle United limefungwa na Matt Ritchie kunako dakika ya 65 ambapo kwa ushindi huo Mourinho anaendelea kuwa na rekodi mbaya kunako Uwanja wa St. James Park ambapo hajawahi kushinda mchezo wowote wa EPL kwenye uwanja huo.
Mourinho akiwa na Manchester United na Chelsea amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi EFL CUP.
Matokeo ya leo yanaiacha Manchester United ikisalia katika nafasi ya pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni kwa pointi 72.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: