Wengi wetu tunapokuwa makazini yapo maisha ambayo  tunakuwa tunaishi na yanapelekea majuto kwa baadae. Maisha haya wanayo wengi sana, hasa vijana wanaopata kazi mapema na kujikuta kujuta baadae.

Unachopaswa kujua au kuelewa, upo msingi wa maisha unatakiwa kuishi nao unapokuwa kazini ili baade usije ukaishi maisha ya majuto na kujilaumu sana hasa pale unapofikia uzeeni kwako.
Katika makala haya itafafanua mambo ya kuzingatia unapokuwa kazini ili maisha yako ya baade yawe ya uhakika na usije ukaishi maisha ya majuto. Sasa twende pamoja ili tuweze kujfunza mambo hayo.

1. Tumia pesa zako kwa busara.
Kwa namna yoyote ile unapokuwa kazini na unapata pesa zako wakati upo kazini, jitahidi sana usiishi maisha ya kujisahau. Watu wengi wanapopata pesa wanakuwa wanajisahau na kujua mshahara kwao ndio kila kitu.

Kwa mfano, utakuta pesa unazipata kweli lakini matumizi yako yanakuwa yako hovyo sana, kiasi kwamba unafika mahali huelewi hata hizo pesa zako unazitumiaje. Kuishi maisha haya ni kutafuta janga kubwa la kushindwa kwa baadae.

Ili kuepuka kuishi maisha ya majuto baade, ishi kwa mipango, pesa zako zipangilie vizuri na ishi kwa kusudi maalumu.

2. Kamilisha mambo yako ya msingi mapema.
Kama unajielewa wewe upo kazini na umeamua kufanya kazi kweli, hebu kamilisha mambo yako mapema. Yapo mambo ya msingi unayotakiwa kuyakamilisha mapema kama vile kusomesha watoto na kujenga nyumba.

Ni kosa kubwa sana, kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kujiandaa kujenga nyumba yako na kusubiri hadi kustaafu kwako. Jenga nyumba mapema, maliza kusomesha watoto wako mapema na usiache jukumu hilo kwa watoto wengine wakajisomesha wao wenyewe.

Unapokamilisha majukumu yako mapema inakupa uhuru  wa kuishi maisha bora pale unapokuwa umestaafu.

Kwa kifupi, hayo ndiyo mamb unayopsw kuyazingatia has pale unapokuw kzaini na wakati huo unajiandaa kutengeneza maisha bora uyatakayo.

Nakutakia wakati mwema na uwe na siku njema, fanyia kazi haya na kila kheri katika kufikia mafanikio yako.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: