Mahakama Kuu nchini Kenya imeiamuru serikali nchini humo kuvirudisha hewani vituo vya runinga vilivyofungiwa Jumanne ya tarehe 30 Januari 2018 kwa makosa ya kurusha tukio la kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga.
Okiya Omtatah
Taarifa za awali zilizotolewa na kituo cha runinga cha NTV kupitia ukurasa wao wa Twitter wamethibitisha hilo.
Government expected to restore NTV, Citizen TV & KTN News signals after High Court suspends switch off for 14 days pending case being heard.
Tamko hilo la Mahakama Kuu limeitaka Serikali kurudisha vituo vya NTV, Citizen TV na KTN News ambavyo vilifungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo kwa siku 14 kuanzia tarehe 30 Januari 2018.

Tamko hilo limekuja baada ya Mwanaharakati Okiya Omtatah kuifungulia kuishtaki Serikali nchini humo juu ya tukio la kuzimwa kwa vituo hivyo vya runinga kinyume na katiba ya Kenya, kesi hiyo itasikilizwa tarehe 14 Februari 2018.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: