Kwa ushindi mnono wa goli 4-1 dhidi ya West Ham United, Klabu ya Liverpool imepanda hadi nafasi ya pili iliyokuwa inashikiliwa kwa muda mrefu na mashetani wekundu Manchester United.
Magoli ya Liverpool yamefungwa na Emre Can, Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino huku goli la kufuta machozi la West Ham likifungwa na Michail Antonio.
Wakati hayo yakijiri mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amefikia rekodi ya Luis Suarez iliyodumu klabuni hapo kwa miaka mitatu, ambapo Suarez aliifungia Liverpool magoli 31 kwa msimu wa mwaka 2013/2014 kwa michezo 37 aliyoitumikia Liverpool hakuna aliyefanya hivyo tangu Suarez aondoke klabuni hapo kwenda Barcelona, hadi jana Salah alipofikisha magoli hayo kwa msimu huu wa 2017/2018.
Salah (25) ameifikia rekodi hiyo mapema zaidi kuliko Suarez sababu ikiwa ni wingi wa michuano ambayo Liverpool ya sasa inashiriki. Tazama matokeo ya mechi nyingine za EPL zilizochezwa jana
Share To:

msumbanews

Post A Comment: